The House of Favourite Newspapers

Zilla Afungukia Mahaba ya Halima Mdee

Golden Mbunda ‘Godzilla’,

 

Hip Hop Bongo, Golden Mbunda ‘Godzilla’, hivi karibuni amefungukia juu ya mahaba aliyooneshwa na Mbunge wa Jimbo la Kawe, Halima Mdee ambaye alimfagilia na kuisapoti kazi yake mpya aliyoitoa ya Ngoma ya Stay.

 

Godzilla alipoulizwa na Risasi Vibes kuhusu Halima kumfagilia na kumsapoti alifunguka: “Kitu kizuri au kazi nzuri hugusa kila nafsi.”

Image result for halima mdee

 

Hata hivyo, Godzilla alipoulizwa juu ya video ya wimbo huo kuchelewa, kwani ni zaidi ya miaka miwili tangu atoe audio ambayo ni ‘cover’ ya wimbo wa mwanamuziki kutoka Marekani, Nasir Jones ‘Nas’ uitwao Stay kutoka kwenye Albamu ya Life Is Good alisema kuwa, kila kitu kina wakati wake.

 

“Kila jambo lina muda wake. Wimbo huu una maudhui yanayoishi na isingekuwa busara kuuacha upite tu!” Alisema Godzilla.

Stori:Boniphace Ngumije

Comments are closed.