The House of Favourite Newspapers

Pigo taifa Stars: Manula, Yondani Kuikosa Algria Leo

Pigo kubwa kwa Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) baada ya kuthibitika kuwa beki kisiki Kelvin Yondani na kipa namba moja Aishi Manula wataukosa mchezo wa leo kati ya Tanzania dhidi ya Algeria kwenye Uwanja wa Al- Salam nchini Misri.

 

Mchezo huo wa mwisho wa Kundi C, hauna maana yoyote kwa Tanzania zaidi ya kusaka kuweka rekodi kwa kuwa wameshatolewa huku Algeria ikiwa imefuzu kama kinara wa kundi hilo.

 

Wachezaji hao wawili wamekosa vipindi viwili vya mazoezi juzi na jana usiku baada ya kuumia katika mchezo dhidi ya Kenya. Daktari wa Taifa Stars, Richard Yomba amesema Yondani na Manula afya zao zimeshindwa kuimarika mapema kabla ya mchezo wa leo usiku.

 

Yomba alisema wawili hao baada ya kupata maumivu katika mchezo dhidi ya Kenya kitengo chake kilipambana kuhakikisha wanakuwa tayari, lakini imeshindikana. Alisema wamelazimika kuwaondoa katika kikosi kitakachocheza mechi ya leo kwa kuwa bado wanaendelea na matibabu zaidi.

Comments are closed.