The House of Favourite Newspapers

Zitto na Lema Waingia Katika Vita ya Maneno

0

Wanasiasa wawili maarufu, Godbless Lema ambaye aliwahi kuwa Mbunge wa Arusha Mjini kwa tiketi ya Chadema, na Zitto Kabwe, kiongozi wa ACT Wazalendo wameingia katika vita ya maneno.

Kupitia akaunti yake ya mtandao wa kijamii wa Twitter, Lema ameandika ujumbe ambao bila kumtaja mtu jina, unamuelezea kijana mmoja ambaye amefananisha na Mwenyekiti wa TLP, Augustino Mrema.

Lema ameandika: “Kuna Kijana mmoja ana-behave na anataka aonekane kama mpinzani wa kweli huku kimsingi yeye ni kama Mrema wa TLP lakini yeye akiwa mchangamfu zaidi.”

Muda mfupi baada ya kupost ujumbe huyo, Zitto Kabwe akaibuka na kuja kuujibu ujumbe huo chini yake, akiandika: “Kijana huyo ndiye aliyekutoa wewe kwa Mrema ukaingia ulipo sasa mwaka 2007. Kijana huyohuyo kwa kushiriakiana na wadau wakiwemo viongozi wako wa sasa ndiyo wataweka mazingira mazuri ya siasa. Endelea wailing sisi tunakuwekea mazingira mazuri ya kufanya siasa.”

Baada ya Zitto kujibu ujumbe huo, wachangiaji wengi wa mitandaoni wakaunganisha picha na kugundua kwamba kumbe aliyelengwa na Lema japokuwa hakuwa amemtaja jina, ni Zitto.

Zitto ni miongoni mwa viongozi wa upinzani ambao wapo katika kamati maalumu iliyoundwa na Rais Samia Suluhu Hassan ya kupitia hoja zilizojitokeza katika mkutano wa wadau wa siasa na vyama uliofanyika mwishoni mwa mwaka jana, mkutano ambao Chadema hawakushiriki.

Leave A Reply