The House of Favourite Newspapers

Zuchu, Eric Omondi Wajibizana Insta

0

MSANII maarufu wa comedy nchini Kenya, Eric Omondi amemjibu msanii maarufu wa Bongo Fleva, Zuchu kufuatia ujumbe alioutuma kama maoni yake kwenye post aliyochapisha kupitia ukurasa wa mtandao wa Instagram wa mchekeshaji huyo maarufu wa nchini Kenya.

Post iliyokuwa na maneno yaliyosomeka ‘AMAPIANO Has Killed BONGO Flavour’ akimaanisha ‘Muziki wa Amapiano umeua muziki wa Bongo Fleva’.

Ujumbe aliouandika kufuatia kukithiri kwa wasanii wa muziki wa Bongo Fleva kujikita katika kufanya aina ya muziki wa asili ya Afrika ya Kusini na kuuacha muziki wa asili ya Tanzania.

Muda mfupi baada ya post hiyo Omondi alipokea maoni (comments) mengi kutoka kwa wadau mbalimbali wa muziki Afrika Mashariki akiwamo Zuchu ambaye aliikosoa vikali kauli hiyo kwa kusema kuwa.

“Muziki wa Bongo fleva hauwezi kufa kamwe, wasanii wanatoka nje ya maeneo yao kutafuta utofauti. Kujaribu mirindimo mipya, hilo halijawahi kuua tasnia yoyote. Tasnia ya muziki ni kubwa sana wacha wasanii wajaribu mambo mapya ndio mabadiliko.”

Eric Omondi amemjibu Zuchu kwa kuandika; “Dada yangu mpendwa, hivi ndivyo inavyoanza, kila mara huwa tunaanza kwa kupoteza uhalisia na utambulisho wetu na kutoa visingizio vyake. Huku Kenya tulianza vivyo hivyo na Muziki wetu ukapotea, Wazungu wanasema “Kama haijavunjwa, usiirekebishe!!.

Bongo Fleva iko sawa kabisa na hakuna haja ya kuwacha Bongo Fleva ati kwa ajili ya ku ‘Diversify‘. Amapiano ni basi tu linalopita ila sisi tukipanda bila kujua linaenda wapi basi tutashindwa kurudi nyumbani.Tutakua tunauza sera zao na Tamaduni zao na kuua chetu.

Unapoimba ‘Sukari’ kwenye hiyo Sweet Authentic Bongo Tone and Beat, unachofanya kimsingi ni Kuinua taifa na bendera ya Tanzania na TUNAIPENDA SANA na tunajivunia.

Lakini when you Continually replace that Bongo Sound na Amapiano baada ya Muda tutakuwa tumejipoteza. Niamini, hii ilitokea kwa muziki wa Kenya, I am Speaking from Experience. Msalimu sana Kaka yangu na wana WCB wote waambie Nawapenda. Naja Dar January nitawaalika show yangu hapo Mlimani City,” ameandika Eric Omondi.

Leave A Reply