The House of Favourite Newspapers

Rais Doumbouya: Rudini na Kombe la AFCON Ama Fedha Zetu

0

RAIS wa mpito wa Guinea, Kanali Mamadi Doumbouya wa Guinea amewaambia wachezaji wa timu ya Taifa hilo kuwa wanatakiwa wachague jambo moja, kurudi na ubingwa wa Afcon2021 au warudishe fedha ambazo serikali imewekeza katika maandalizi ya timu hiyo ya Taifa.

“Rudini na kombe au fedha tulizoziwekeza kwenu,” alisema Doumbouya. Doumbouya ametoa kauli wakati akiwakabidhi bendera wachezaji wa timu ya Taifa ya Guinea inayoenda kushiriki AFCON 2021 nchini Cameroon.

Guinea ni mojawapo ya nchi zinazoshiriki kombe la Afrika (AFCON) huko nchini Cameroon, asubuhi ya leo walikabidhiwa bendera ya Taifa na Kanali Mamadi Doumbouya. Ikumbukwe Doumbouya aliingia madarakani baada ya jeshi kuipindua serikali ya kiraia ya nchi hiyo.

Leave A Reply