The House of Favourite Newspapers

Akinamama Waandaa Shughuli Kunusuru Ndoa Zao

0
Anti Sadaka akiongea na wanahabari (hawapo pichani).

AKINAMAMA nchini wanatarajia kukutana na kujadili masuala ya kulinda ndoa zao katika kongamano liitwalo VIP Ndoa linalotarajiwa kufanyika Desemba 15 mwaka huu kwenye Jengo la City Mall, Dar.

 

Akizungumza na wanahabari, mkufunzi wa masuala ya saikolojia na mahusiano, Sadaka Gandi, maarufu kama Anti Sadaka, amesema kutokana na migogoro mingi ya ndoa katika kongamano hilo kina mama watapata somo la kulinda ndoa zao.

Anti Sadaka akiwa na waandaji wenzake wakati wa kongamano hilo.

Ameongeza kwamba kutakuwa na walimu kutoka Kenya na Burundi ambao nao wataeleza changamoto za ndoa nchini mwao na hivyo kushirikiana  kupata utatuzi.

 

HABARI:NEEMA ADRIAN

PICHA:RICHARD BUKOS/GPL

Leave A Reply