The House of Favourite Newspapers

Azam kupewa kombe na TFF

0

Azam Ngao ya jamii

Wachezaji na Viongozi wa Azam wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kukabidhiwa kombe ambalo halikuwa lenyewe.

Said Ally Dar es Salaam
SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) limeweka bayana kuwa, lipo kwenye mpango wa kuwakabidhi kombe jipya la Ngao ya Jamii timu ya Azam kutokana na kukabidhiwa kombe ambalo halikuwa lenyewe.

Azam waliichapa Yanga kwa penalti 4-1 katika mchezo wa Ngao ya Jamii baada ya kumaliza dakika tisini kwa sare ya mabao 2-2, kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar.

IMG_0391

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba (kushoto) akikabidhi  Ngao ya Jamii John Bocco ‘Adebayor’.

Msemaji wa TFF, Alfred Lucas ameliambia Championi Jumatano kuwa, waliwapa Azam ngao ambayo siyo yenyewe kutokana na kuchelewa kukamilika kwa utengenezwaji wa ngao halali ambayo walitakiwa kupewa.
“Lile kombe ambalo tuliwapa Azam siku ile walipocheza na Yanga kwenye Ngao ya Jamii halikuwa lenyewe, bali tulilitoa kwa ajili ya kuziba nafasi ya kombe halisi ambalo lilichelewa kuja kutokana na kutokamilika mpaka inafika siku ile, hivyo tukaona siyo vizuri bingwa akiondoka mikono mitupu.
“Tumepanga kuwabadilishia na kuwapa kombe lao halisi ambalo walistahili kupewa ambalo hili litakuwa na thamani halisi na mwonekano tofauti kabisa na lile ambalo tulilitoa awali,” alisema Lucas.

Leave A Reply