The House of Favourite Newspapers

Dayna: Nilipisha uchaguzi kwanza

11187081_1573877289553148_1772098098_n (1)Dayna Nyage.

MSANII wa Kike anayefanya poa katika Bongo Fleva, Dayna Nyage amefunguka juu ya kucheleshwa kutoa video ya wimbo wake mpya wa ‘Nitulize’ aliomshirikisha msanii mwenzake Nay wa Mitego kuwa alifanya hivyo ili kupisha uchaguzi mkuu.

Akichonga na paparazi wetu, Dayna alisema anafahamu mashabiki wake wana hamu na video hiyo ambayo amepania kufanya vizuri.

“Uongozi wangu ulibadilisha ratiba ya kushoot video hiyo ili kupisha uchaguzi upite, kwa sasa kila kitu kimekamilika ila siku ya kuzindua rasmi siitaji maana nataka iwe sapraizi, mashabiki wakae mkao wa kula tu,” alisema Dayna.

Comments are closed.