The House of Favourite Newspapers

EXCLUSIVE: ZAHERA Ataja OFA Alizopata – “SIMBA Naweza Kwenda, Mimi ni KOCHA”- Video

KOCHA ambaye jina lake likitajwa tu mashabiki wa Yanga wanashtuka, Mwinyi Zahera ametua nchini usiku wa kuamkia jana Jumatano. Zahera tofauti na alivyozoeleka juzi alikuwa amepiga uzi mwekundu wa timu ya Taifa ya DR Congo na baadhi ya mashabiki waliokuwa kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere aliwagawia.

 

Yanga wamekuwa hawataki kumsikia Zahera kwa madai kwamba anavujisha siri zao kwenye vyombo vya habari. Spoti Xtra linajua kwamba kocha huyo ana ofa tatu mezani kwake ingawa amegoma kuweka wazi majina ya timu mpaka atakapomalizana na Yanga wiki ijayo…Soma zaidi kwenye gazeti la SPOTI XTRA la leo Novemba 28, 2019

Comments are closed.