The House of Favourite Newspapers

Global TV Yamfungia kazi ‘Bi Harusi’ wa picha za utupu, hii hapa video akifunguka

1

GGGDDGLydia John Njau kijiachia ‘kima-lovee’ na kijana aliyemtaja kwa jina moja la Vincent.

Na Waandishi Wetu, RISASI Mchanganyiko

DAR ES SALAAM: Imefichuka sasa! Baada ya kusambaa kwa picha za utupu mitandaoni zikimuonesha mrembo akifanya ngono isiyoelekezwa na Muumba na kudaiwa picha hizo zilisababisha kuvunjika kwa ndoa ikiwa kwenye fungate, Lydia John Njau, ameibuka na kuzungumzia sakata hilo huku akimtaja mbunge mmoja alichomtenda kufuatia sakata hilo.

SAMSUNG CAMERA PICTURESLydia akiwa ndani ya ofisi za Global Publishers.

Lydia, alisema kuwa, baada ya picha hizo kusambaa mtandaoni, mbunge huyo kutoka katika jimbo moja kanda ya kaskazini ambaye alikuwa rafiki yake wa kawaida kwenye Facebook, alimuita kumfuata akisema atamfariji na kumpa njia ya nini cha kufanya katika kipindi hiki kizito kwake, lakini matokeo yake hakuweza kuutua mzigo wa kashfa ya picha.

MAPICHAZ (1) Moja ya picha zake chafu zilizovuja

KWANZA AKIRI KUHUSU PICHA

Awali, Lidya mama wa watoto wawili alikiri mbele ya kamera za Risasi Mchanganyiko kuwa, ni yeye ndiye anayeonekana katika baadhi ya picha lakini zilizounganishwa na kutupiwa mitandaoni na kijana aliyewahi kuwa ‘boyfriend’ wake.

MSIKIE MWENYEWE

“Ninamfahamu Vincent, alikuwa mwanaume wangu kwa kama mwaka mmoja nyuma. Nnakumbuka siku tunapiga picha hizo tulilala wote sehemu moja inaitwa Fimbo Guest House, Mbagala (Dar). Hakunilazimisha, nilipiga mwenyewe kwa furaha kabisa, nilifanya hivyo kwa kumuonesha upendo tu (show love) na si vinginevyo.”

SAMSUNG CAMERA PICTURESKWA HIYO PICHA ZOTE NI ZAKE?

“Hapana, hizi zingine zote (anazionesha zilizopigwa chumbani Fimbo Guest House) ni zangu, ndizo tulizopiga siku ile, hizi mbili (zile za ngono isiyoelekezwa na Muumba) si zangu, hata ukitazama mazingira ya chumba na rangi ya mwili na umbo la huyu mwingine, si mimi.

“Picha hizi zilipigwa sehemu nyingine, zikaunganishwa hapa, sijui kwa nini. Sijawahi kufanya huu mchezo hata mara moja, naona nia yake ilikuwa ni kunichafua tu.”MAPICHAZ (2)

WALIWAHI KUGOMBANA NA VINCENT?

“Ndiyo, kuna wakati nilimwambia sitaki tena uhusiano naye kwa sababu alimtongoza ndugu yangu. Huyo ndugu yangu akaniambia mbona Vincent ananitongoza wakati ni mtu wako? Nikamwambia kwa nini anafanya hivyo, anataka kutuchanganya mimi na ndugu yangu? Nikaamua kuachana naye.

“Siku moja alipeleleza ninapokaa Mbagala, akaja. Ilikuwa usiku, akagonga nikamfungulia bila kujua kama ni yeye, akamkuta mbaba mmoja hivi ambaye nilikuwa natembea naye wakati huo, akamuuliza mimi ni nani yake, yule mbaba akamwambia aniulize mimi, aliponiuliza nikamwambia ni mtu wangu.

“Akatoka huku akamwambia yule baba kuwa anaondoka lakini lazima ajue kuwa hajaniacha, alipoondoka na yule mzee akaondoka, wakaenda kukutana Kizuiani (Mbagala pia), ndipo akamuonesha zile picha akisema mimi ni mtu wake wa kila siku, kitendo kile kilimuudhi sana yule mzee akaamua kuniacha.”

SAMSUNG CAMERA PICTURESALIWASILIANA NAYE BAADA YA KUVUJISHA PICHA?

“Ndiyo, nilimpigia simu Vincent na kumuuliza, akasema eti simu yake iliibwa, nikamuuliza kwa nini alikaa na picha zile kwa muda mrefu tofauti na makubaliano? Akajizungusha na kukata simu. Tokea wakati huo sijampata tena hewani.

“Lakini baada ya kusambaa mitandaoni sana na kupigiwa simu na watu mbalimbali, wakiwemo ndugu, niliamua kwenda kushitaki Kituo cha Polisi Kizuiani, cha ajabu baadhi ya askari wakasema hata wao wanazo picha hizo kwenye simu zao, wakaandikisha maelezo yangu na kusema wanaendelea na uchunguzi.”

VIPI KUHUSU NDOA YAKE?

“Sijawahi kuchumbiwa wala kuolewa, sina uhusiano wowote na hiyo ndoa inayosemwa ilivunjika maharusi wakiwa fungate kwa sababu ya picha na wala sijawahi kuhojiwa na chombo chochote cha habari zaidi ya leo nilivyokuja hapa Global.”

NA ILE SAUTI MITANDAONI?

“Nadhani imeunganishwa tu, anayezungumza katika ile sauti iliyopo mitandaoni siyo mimi, hilo tukio linalosemwa halihusiani na mimi, litakuwa limewatokea watu wengine.”

KUHUSU MBUNGE?

“Kuhusu huyo mbunge ni kwamba, kwa sababu alikuwa rafiki yangu wa Facebook, alipoona picha zangu chafu mitandaoni, alichukua moja nikiwa nimelala mtupu kitandani, akanitumia na kuniuliza ni wewe kweli?

“Nilimjibu ni mimi na kumwambia namna nilivyochanganyikiwa, akasema niachane na mawazo ya picha hizo, niende….(anakutaja jina) ili akanifariji na kunielekeza namna ya kuondoa mawazo hayo.

“Kusema ukweli, kwa mzigo mkubwa wa mawazo niliyokuwa nayo, maana nilitamani hata kujiua, nilijikuta nakubali kushauriwa na kila mtu. Hivyo, mbunge alinitumia shilingi 100,000 ili nimfuate. Nilipanda basi, nikaenda. Nikawa naye kwa siku tatu, lakini kusema ukweli sikuona faraja yoyote ile zaidi ya maumivu kuzidi kwani picha zilizidi kusambaa, watu walizidi kunipigia simu, wengine wakinipa pole, wengine wakinishangaa.”

KUHUSU GLOBAL?

“Kusema kweli kwanza nawapongeza sana Global kwani hamkutaka kukurupuka kuiandika habari yangu kwa kutumia picha tu za mtandaoni. Mmefanya bidii kunitafuta na kuniita hapa ofisini kwenu ili jamii ijue ukweli. Na ukweli ndiyo huo, mimi si mke wa mtu, sina ndoa iliyovunjika kwenye fungate,” alimalizia Lydia.

Bofya==>Picha chafu zavuja na kuvunja ndoa ya wiki moja!

‘Bi Harusi’ wa picha za utupu, hii hapa video akifunguka!-Part 01

‘Bi Harusi’ wa picha za utupu, hii hapa video akifunguka!-Part 02

1 Comment
  1. Athumani nya2ru says

    msiwe mnakubali kupigwapigwa picha ovyo wadada.

Leave A Reply