The House of Favourite Newspapers

Kabendera Atakiwa Kwenda ‘Kubageini’ na DPP

0

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imeuambia upande wa utetezi katika kesi ya uhujumu uchumi inayomkabili mwandishi wa habari za uchunguzi, Erick Kabendera, kuwa waende wenyewe kwa Mkurugenzi wa Mashtàka nchini (DPP) ili kujua hatma ya barua ya mshtakiwa ya makubaliano ya kuomba msamaha na kukiri kosa (pre-bargaining).

 

Hatua hiyo imefikiwa wakati kesi hiyo ilipoitwa mahakamani hapo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Janet Mtega, kwa ajili ya kutajwa na kudaiwa kuwa upelelezi bado haujakamilika hivyo upande wa utetezi wakawasilisha hoja zao.

 

Wakili wa utetezi Jebra Kambole alidai mahakamani hapo kuwa, Oktoba 11, 2019, waliitaarifu mahakama juu mshtakiwa kuandika barua ya kuomba msahama na kukiri kosa kwenda kwa DPP lakini mpaka leo ni miezi miwili hawajapata mrejesho wowote kutoka kwa DPP.

 

Akijibu hoja hizo wakili wa serikali, Ester Martin, amekiri kwamba ni kweli maombi yao hayo yapo kwa DPP toka Oktoba 11 hadi leo lakini suala la makubaliano si maamuzi yanayoweza kutolewa mara moja, ni vema waende katika ofisi ya DPP ili wajue kinachoendela.

 

Hakimu Mtega naye amesema, kufuatia hoja hizo, amewataka upande wa utetezi waende wenyewe kufuatilia jalada la kesi kwa DPP ili wajue kinachoendelea na ameiahirisha kesi hiyo hadi itakapotajwa tena Desemba 18, mwaka huu.

 

Katika kesi hiyo, Kabendera anakabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi yenye mashtaka matatu likiwemo la utakatishaji wa Sh milioni 173.

 

Leave A Reply