The House of Favourite Newspapers

Kessy ndiye anayempa jeuri Kiiza

0

Hassan-‘-Kessy’-Ramadhani2 Beki wa Simba, Hassan Kessy.

Sweetbert Lukonge,
Dar es Salaam
STRAIKA wa Simba, Hamis Kiiza ndiye anayeongoza kwa kuzifumania nyavu katika Ligi Kuu Bara akiwa na mabao 14 sawa na Amiss Tambwe wa Yanga.

Siri kubwa nyuma ya mabao ya Kiiza raia wa Uganda ni kwamba, mpishi wake mkuu ni beki wa kulia wa timu hiyo, Hassan Kessy ambaye amempa pasi za mwisho tano hadi sasa.

kiiza-akishangilia-baada-ya-kutikisa-nyavu-uwanja-wa-taifa-dar-es-salaam_f9e7nzxc6j531t6oujg70lpkp Straika wa Simba, Hamis Kiiza.

Akizungumza na Championi Jumamosi, Kessy alisema nafasi hizo ni zile tu ambazo Kiiza kazitumia vizuri na kufunga lakini pia amemtengenezea nyingine nyingi ambazo hakufunga.
“Najivunia hali hiyo kwani inanifanya nijisikie mwenye furaha muda wote, lakini pia Kiiza naye anajiona mwenye furaha kwa kuwa na uhakika mkubwa wa kufunga katika kila mechi anazocheza.
“Namuomba Mungu anijalie afya njema ili niweze kundelea na kazi yangu hiyo, pia namuomba Kiiza na washambuliaji wengine wote katika kikosi chetu wazidishe umakini,” alisema Kessy.

Leave A Reply