The House of Favourite Newspapers

Mbatia: Rais Apeleke Muswada Bungeni Kufuta Vyama vya Siasa

0

Mbatia (1)    

Mwenyekiti wa Chama cha NCCR Mageuzi Taifa, James Francis Mbatia (wa pili kushoto) akizungumza na wanahabari (hawapo pichani).

Mbatia (2)

Mbatia (wa pili kushoto) akionesha hisia zake mbele ya wanahabari.

Mbatia (5)

Mkutano ukiendelea.Mbatia (4)

Wanahabari wakichukua tukio hilo leo Agosti 25, 2016.

Mbatia (5)

Baadhi ya viongozi wa vyama vya upinzani wakisikiliza maswali kutoka kwa wanahabari.

NA DENIS MTIMA

MWENYEKITI wa Chama Cha NCCR Mageuzi Taifa, James Francis Mbatia amemtaka Rais Dk. John Pombe Magufuli kupeleka muswada bungeni katika kikao kijacho cha Bunge ili kuandaa sheria ya kuvifuta vyama vyote vya siasa na kuangalia kile ambacho yeye anaona kitafaaa kuiongoza serikali bila migogoro kama inayojitokeza sasa.

Hayo ameyasema leo katika makao makuu ya chama hicho yaliyopo Ilala-Bungoni jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na wanahabari.

Mbatia alisema kuwa, Rais Magufuli hawezi kukinzana na upinzani uliopo kwa sasa kwa kuzuia mikutano na maandamano wanayotaka kufanya kwa kuwa yanakubalika kisheria.

Alisema, msimamo wa chama chake na vyama vingine vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA), azma yao iko palepale ya kufanya maandamano ya amani nchi nzima ifikapo Septemba Mosi mwaka huu kupitia umoja wao waliouita UKUTA.

Ili kupata hotuba nzima ya alichokisema Mbatia tembelea www.globaltvtz.com au Subscribe Youtube Channel ya Global TV Online.

 

Video: Kauli ya Mbatia

Leave A Reply