The House of Favourite Newspapers

Wasomaji wa Amani, Tandika Wachangamkia Safari ya Dubai

0

1Stela Hema (aliyeshika gazeti) akiwa anasoma Gazeti la Amani na wenzake, kulia ni ofisa usambazaji Jimmy Haroub. 2      Ofisa usambazaji, Yohana Mkanda (kulia) akiwa na wasomaji wakifuatilia jambo kwenye Gazeti la Amani.

3Charles Kalembo,Mohamed Seleman na Hassan wakazi wa Mbagala wakisoma magazeti ya Amani.

4Shamsa Musa mkazi wa Mbagala akisoma Gazeti la Amani.

5Salehe Mgalula mkazi wa Kijichi akifuatilia kwa makini habari zilizoandikwa kwenye Gazeti la Amani.6

Mwanahawa Sandali mkazi wa Tandika akisoma Gazeti la Amani.

7Muuzaji wa Gazeti la Amani, Abdulmalick (kulia) akikabidhiwa kuponi na ofisa usambazaji.

8Steve muuzaji wa Gazeti la Amani maeneo ya Karume (kulia) akikabidhiwa kuponi.

 

WASOMAJI wa Gazeti la Amani katika mitaa ya Kijichi, Tandika, Mbagala na maeneo mengine ya Jiji la Dar es Saalaam, leo wamejitokeza kwa wingi kulichangamkia gazeti hilo ambapo wameonesha kuvutiwa na Chemsha Bongo ya kwenda Dubai.

Timu ya gazeti hilo ilitinga kama kawaida maeneo hayo kwa lengo la kuonesha wasomaji mabadiliko makubwa yaliyofanywa ndani ya gazeti hilo ikiwa ni sambamba na kuwepo kwa safu mpya kama vile Kijiwe cha MC Pilipili, Nafasi za Kazi, Sindano za Mastaa, Mtu Kati na nyingine nyingi.

 “Jamani nalipenda sana Gazeti la Amani kwani ndilo  gazeti bora hapa Bongo kwa sasa lenye habari zake za kuvutia za wasanii mbalimbali, habari zake, hadithi na makala zinanifanya nisiache kulinunua,” alisema Salehe mkazi wa Kijichi.

Aidha msomaji wa gazeti hilo unaweza kushiriki katika chemsha Bongo iliopo ukurasa wa pili katika gazeti hilo na kujishindia kuanzia Sh. 500,000 hadi tiketi ya kwenda Dubai na kuponda raha katika hoteli ya kifahari kwa muda wa siku tatu.

Wiki iliyopita mshindi wa chemsha bongo, Bakari Omari mkazi wa Manzese, Dar alijipatia zawadi ya shilingi laki tano na kukabidhiwa katika ofisi za gazeti hili zilizopo Bamaga-Mwenge jijini Dar.

Naye Mhariri wa gazeti hilo, ameendelea kutoa wito kwa wasomaji wa Magazeti ya Global Publishers ya Ijumaa Wikienda, Risasi, Amani na Championi, isipokuwa Ijumaa linalouzwa Sh.1000,  kuendelea kulinunua Amani kwa bei ya Sh.500 kwani thamani ya kilichomo ndani yake ni zaidi ya bei hiyo.

Stori/picha: Gladness Mallya/GPL

Leave A Reply