The House of Favourite Newspapers

Mkuki Moyoni Mwangu- 39

0

CATARINA hajulikani aliko, familia yake imechanganyikiwa, mchumba wake, Kevin amefikia uamuzi wa kukatisha masomo yake Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ili asafiri hadi Paris, Ufaransa, kwenda kufuatilia. Anataka kuufahamu ukweli juu ya mahali aliko Catarina, kwani awali ilijulikana kwamba alivunja mkataba na Kampuni ya Fonex Modelling ya Afrika Kusini na kusafiri na wakala aitwaye Mario Pizaro, kuelekea New York, Marekani alikoahidi kwenda kumtafutia kazi kwenye kampuni nyingine ya uanamitindo.

Cha kushangaza, Mario Pizaro alipohojiwa na afisa wa ubalozi, alikana kusafiri na Catarina kutokea Paris, akidai wakiwa uwanja wa ndege Catarina alibadilisha mawazo na kuamua kubaki Ufaransa ili arejee Afrika.

Kevin ameshindwa kuyaamini maneno hayo, anahisi Catarina ameuawa kwa sababu alikuwa tishio katika ulimwengu wa mitindo ndani ya muda mfupi.

Ukweli unaofichwa ni kwamba Catarina alisafiri na Mario Pizaro ndani ya ndege ya tajiri Jackson Motown ambaye aliapa kwa Catarina kwamba atake asitake lazima siku moja angekuwa mke wake, alishambaka mara ya kwanza pale wakala Craig alipomuuza kwake nchini Afrika Kusini! Wakiwa angani, Catarina alipewa taarifa kuwa tajiri ambaye angempa kazi huko New York, alitaka kuongea naye, dakika tano baadaye akiwa hajui kinachofuata, alimwona Jackson Motown akiingia tena utupu!
Kilichoendelea ndani ya ndege hiyo kilikuwa ni kubakwa Catarina akiwa amegandamizwa kitandani na mlinzi wa Motown mpaka akapoteza fahamu, wakamtingisha kwa muda mrefu lakini hakuzinduka, hofu yao ikawa huenda alikuwa amekufa.

Kevin amewasili Paris, alipotoka tu nje ya uwanja alikutana na dereva wa teksi na kumtaka ampeleke kwenye hoteli ya bei rahisi, wakiwa njiani mazungumzo yaliendelea…

Je, nini kitafuata? Atafanikiwa kuujua ukweli? Catarina yuko hai ama amekufa?
SONGA NAYO…

“DO you speak English?” (Unaweza kuongea Kingereza?)
“je ne parle anglais” Alijibu dereva wa teksi kwa Lugha ya Kifaransa akimaanisha, lugha hiyo haifahamu.
“Hotel! Nearby, cheap!” (Hoteli ya bei rahisi iliyo karibu!) Kevin aliongea kwa maneno ya Kingereza ambayo ni rahisi kuyaelewa lakini bado dereva wa teksi hakuelewa mpaka dereva mwingine mwenye kuzungumza Kingereza kidogo alipowasogelea na kumchukua Kevin baada ya kumwelewa.
“Where are you from?” (Unatokea wapi?)
“Tanzania.”
“Ooh! Tanzania? Good country, huh?” (Ooh! Tanzania, nchi nzuri, sivyo?)
“Yes!” (ndiyo!)
“I am from Algeria, I have lived in Paris for 25 years!” (Mimi natokea Algeria, nimeishi hapa Paris miaka ishirini na tano!)
“What is your name?” (Jina lako nani?)
“Abou Mohamed!”
“Good to know you!” (Nimefurahi kukufahamu!)
“Welcome to Paris, I will be your good driver, okay?” (Karibu Paris, nitakuwa dereva wako mzuri, sawa?)
Alipelekwa hadi nje kidogo ya Jiji la Paris kwenye kitongoji kiitwacho Chatou, huko ndiko alifanikiwa kupata nyumba ya kulala wageni ya dola thelathini kwa usiku mmoja, akachukua chumba na kuagana na dereva teksi kwa ahadi kwamba wangekutana asubuhi siku iliyofuata.
Usiku mzima hakulala akijaribu kuchunguza mahali pa kuanzia, alipita mtandaoni akifuatilia onyesho la Mavazi la Paris ambalo Catarina alikuja kushiriki hapo Ufaransa, picha zake zilimvutia, alikuwa amebadilika na kuwa msichana mrembo kupita kiasi, haikuwa rahisi kwa Kevin kuamini mtu aliyekuwa akimwona kwenye picha mtandaoni ndiye aliyewahi kuugua saratani ya damu, akamwokoa kwa kumpa uboho wake.
“Lazima nimpate, naomba Mungu tu wawe hawajamuua!”
Katika pekua zake mtandaoni alifanikiwa kugundua kuwa kampuni iliyoandaa onyesho la mavazi iliitwa Paris Fashion Week na ofisi zao zilikuwa katikati ya Jiji la Paris, kitu cha kwanza alichokifanya asubuhi baada ya dereva wa teksi kufika ni kumwonyesha jina la kampuni hiyo, kabla hata hajasema chochote dereva alimuuliza kama hapo ndipo mahali alipotaka kwenda.
“Yes!” (ndiyo!)
“I know the place, I know Paris like the back of my palm because I have lived here 25 years!” (Napafahamu, naijua Paris kama nyuma ya kiganja cha mkono wangu, nimeishi hapa miaka ishirini na tano!)
“Let’s go!” (Twende!)
Ilikuwa ni safari ya dakika arobaini na tano mpaka kufika mbele ya jengo refu ambalo kwa juu liliandikwa Meridien, wakaegesha kwenye maegesho na Kevin kushuka akimwacha dereva Abou kwenye gari akatembea kwa kasi hadi mapokezi ambako aliomba kuonana na mkurugenzi.
“Avez-vous un rendez-vous avec lui” (Una miadi naye?) aliuliza msichana huyo, alipogundua Kevin hamwelewi akaongea kwa Kingereza kibovu huku akichanganya na ishara za mikono.
“No!” (Hapana!)
“Vous ne pouvez pas le voit!” (Huwezi kumwona!)
“Tell him I am Catarina’s relative from Africa.” (Mwambie natokea Afrika, ndugu yake na Catarina David!)
“Attendez!” (Subiri!) aliongea msichana huyo akinyanyua mkono wa simu kisha kupiga namba fulani ambazo Kevin hakuzitambua, kwa Kifaransa akaongea maneno mengi akionekana kutoa maelezo ya mgeni aliyekuwa mbele yake.
Alipokata simu alimwonyesha Kevin kiti na kumtaka aketi, akakusanya ngumi za mikono yake miwili pamoja kuonyesha ishara kwamba alitakiwa asubiri kwa dakika kumi, muda huo ulipofika akachukuliwa na kupelekwa ofisini kwa mkurugenzi ambaye baada ya salamu na utambulisho, sababu aliongea Kingereza kizuri, maongezi kati yao yaliendelea, Kevin akitaka kufahamu mahali Catarina alipokuwa.
“She left with Mario to New York!” (Aliondoka na Mario kwenda New York!)
“No! Mario claims that, Catarina changed her mind at the airport!” (Hapana! Mario anadai kwamba Catarina alibadilisha mawazo yake uwanja wa ndege!)
“And she stayed in Paris?” (Akabaki Paris?)
“Yes!” (Ndiyo!)
“That’s a lie and I can prove it!” (Huo ni uongo na ninaweza kuuthibitisha!)
“How?” (Kuuthibitishaje?)
“Come with me!” (Nifuate!)
Akamfuata nyuma hadi nje ambako Kevin aliingia kwenye gari la tajiri Piere Botui, alichokifanya ni kumwonyesha ishara dereva wake awafuate nyuma, safari yao ikaanza na kuishia Uwanja wa Ndege wa Charles De Gaulle jijini Paris Piere kwa ushawishi wake akaweza kuingia mpaka kwa meneja wa uwanja na kumweleza sababu ya uwepo wao ofisini kwake.
“Let’s go and check the security cameras footage at airport to see if she left or not!” (Twendeni tukaangalie kwenye kamera za uwanja kuona kama aliondoka ama alibaki tutaona!)
Wote wakaongozana mpaka kwenye chumba cha kamera za usalama wa uwanja, kumbukumbu zikarudishwa nyuma mpaka siku Mario Pizaro alipoondoka Paris, kila kitu kilionekana wazi akiwa na Catarina, wakaingia ndani ya ndege binafsi, ikaruka na kupotelea angani.
“Mario Pizaro anafahamu mahali Catarina alipo, yeye ndiye anahusika na kupotea kwake, kesho naondoka kuelekea New York, huko ndiko nitajua ukweli wa mambo!” Kevin alijisemea moyoni mwake.

Je, nini kitaendelea? Kevin atafanikiwa kumpata Catarina akiwa hai? Fuatilia siku ya kesho katika Gazeti la Championi Jumamosi.

HADITHI ZA KUSISIMUA NA MBINU ZA UJASIRIAMALI, INGIA NA LIKE PAGE YA FACEBOOK YA ERIC SHIGONGO===>https://www.facebook.com/shigongotz/

KWA HABARI ZA KITAIFA, KIMATAIFA, MASTAA NA MIKASA YA KUSISIMUA TUFOLLOW

INSTAGRAM===>https://www.instagram.com/globalpublishers/

TWITTER===>https://twitter.com/GlobalHabari

FACEBOOK===>https://www.facebook.com/GlobalPublishers

YOU TUBE===>https://www.youtube.com/user/uwazi1

Leave A Reply