The House of Favourite Newspapers

Satarani ya matiti (Breast Cancer)

0

breastcancerillustrationsLeo tutajadili ugonjwa wa kansa ya matiti unaowashambulia zaidi wanawake. Kuna mambo kadhaa ambayo yameonekana kuwa na uhusiano, ama wa moja kwa moja au usio wa moja kwa moja wa kusababisha saratani ya matiti, au kumfanya mtu au kundi la watu kuwa katika hatari ya kupata ugonjwa huu kuliko wengine.

Ingawa saratani ya matiti huweza kuwapata wote wanawake na wanaume, lakini imeonekana kuwa wanawake ni waathirika wakubwa zaidi wa saratani hii kuliko wanaume.

Uwezekano wa kupata saratani hii huendana na umri wa mtu. Kadiri umri wa mtu unavyoongezeka ndivyo pia uwezekano wa kupata saratani hii unavyozidi kuwa mkubwa. Wanawake walio na umri wa kuanzia miaka 50 wapo kwenye hatari kubwa mara 2 au 3 zaidi kuliko walio na umri wa miaka 45.

Wanawake ambao hawajazaa au kunyonyesha wapo kwenye hatari zaidi ya kupata saratani ya matiti. Wanawake wanaopata ujauzito kwa mara ya kwanza baada ya miaka 30 nao pia wapo kwenye hatari kubwa ya kupata ugonjwa huo.

Wanawake ambao familia zao zina historia ya ugonjwa huu wana uwezekano mkubwa wa kupata saratani ya matiti ikilinganishwa na wale ambao hawana historia ya ugonjwa huu katika familia zao.

 Kwa mwanamke aliye na ndugu (mama, dada au mtoto) ambaye aliwahi kupata saratani hii kabla ya umri wa miaka 50, uwezekano wa mwanamke huyo kupata ugonjwa huu ni mara mbili ya yule ambaye hana historia hii.

Wanawake wanaovunja ungo kabla ya umri wa miaka 12 wapo kwenye hatari zaidi ya kupata ugonjwa huu. Kwa kawaida wanawake huacha kupata hedhi kuanzia miaka 45, hali ambayo kitaalam hujulikana kama Menopause. Wanawake wanaochelewa kuacha kupata hedhi, kwa mfano wale wanaoendelea kupata hedhi wakiwa na zaidi ya miaka 45, wapo kwenye hatari kubwa zaidi ya kupata kansa ya matiti.

Leave A Reply