The House of Favourite Newspapers

Yanga Yasonga Mbele Michuano ya CAF

0

YANGA (3)

Donald Ngoma akimtoka mchezaji wa Sagrada Esperanca.

YANGA (4) YANGA (5)

Kipa wa Yanga, Dida akiokoa hatari langoni mwake.

YANGA (6) YANGA (7)

Amissi Tambwe akiwania mpira na mchezaji wa Sagrada Esperanca.

YANGA (8) YANGA (9)

Sagrada Esperanca wakishangilia bao lao dakika ya 25.

YANGA (10)

Mbuyu Twite kazini.

YANGA (11)

Donald Ngoma (juu) akijaribu kuwatoka wachezaji wa Sagrada Esperanca.

YANGA (12)

YANGA (2)

Kikosi cha Sagrada Esperanca.

YANGA (1)

Mashabiki wa Sagrada Esperanca.

YANGA imesonga mbele kwenye hatua ya makundi katika michuano ya CAF mbali na kipigo cha bao 1-0 kutoka kwa Sagrada Esperanca katika mchezo wao wa leo.

Kikosi hicho cha Jangwani kimefuzu kwa matokeo ya jumla ya 2-1.

Katika mechi hiyo iliyopigwa nchini Angola, Sagrada Esperanca walipata bao dakika ya 25 ya mchezo kupitia kwa mshambuliaji wao, Love Kabungula aliyeunganisha krosi baada ya mabeki Yanga kushindwa kuuwahi mpira.

Aidha katika mechi hiyo, nahodha wa Yanga Nadir Haroub Cannavaro alizawadiwa kadi nyekundu dakika za mwisho za mchezo huo huku Sagrada Esperanca wakipata penalti iliyookolewa na kipa wa Yanga, Dida.

PICHA ZOTE NA MUSA MATEJA / GPL, ANGOLA

Leave A Reply