The House of Favourite Newspapers

Video: Shigongo Afundisha Jinsi Ya Kupata Watoto Wenye Akili!

0

MHAMASISHAJI na Mkurugenzi wa Makampuni ya Global Group, Eric Shigongo, ametoa darasa mahsusi kwa wazazi ili waweze kupata watoto wenye akili.

Akizungumza kupitia kipindi cha Darasa kinachorushwa +255GlobalRadio, Shigongo aisema, ili wajawazito waweze kuzaa watoto wenye akili, wanapaswa kuacha baadhi mambo ili waweze kujifungua watoto wenye akili.
“Hakuna kitu muhimu kama kuona kilichoko mbele ni kikubwa kuliko unachotakiwa kukifanya sasa, ni lazima uache jambo fulani ili uweze kupata kikubwa kilichoko mbele, uking’ang’ania tabia fulani utapoteza kitu kikubwa,” alisema Shigongo na kuongeza:

“Mama lazima awe tayari kuacha vitu anavyovipenda ili aweze kuhakikisha mtoto wake anazaliwa akiwa na uwezo mkubwa wa akili kwa sababu akiendekeza hiki kitu ambacho ni kiu tu inamsumbua atapata mtoto ambaye mwisho wa siku hataweza kuleta furaha kwenye familia yake.”

Shigongo alisema, kuna vitu kama pombe, na vitu vingine ambavyo wamama wanashauriwa kuacha kuvitumia, ni vizuri wakajitahidi kuviacha lakini hata wakijifungua, vipo vitu vya kufanya unavyotakiwa kuvizingatia.

“Hakuna kitu muhimu kama mtoto akizaliwa kunyonyeshwa yale maziwa ya mwanzo yale mazito.

Yale mazito ambayo kina mama wengi huwa wanayakamua wanayamwaga halafu wanaanza kumnyonyesha mtoto maziwa masafi,” alisema Shigongo huku akisisitiza kwamba anayasema hayo kwa sababu ya kujifunza vitu vingi kwenye mitandao.

Ili kutazama mahojiano kamili, ingia kwenye YouTube, itafute GlobalTV Online.

 

Leave A Reply