The House of Favourite Newspapers

Rais Samia Ashtukiza Soko la Kariakoo, Asimamisha Uongozi -Video

0

Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan leo Juni 1, 2021 amefanya ziara katika la Kariakoo jijini Dar es Salaam na ameagiza kusimamishwa kazi kwa viongozi wa soko hilo kupisha uchunguzi.

“Ndugu zangu nimeona nije nione pahali ambapo watanzania wengi wanafanya biashara..”.

 

“Nimeona Serikali itusaidie kwanza kuendesha soko hili, hali niliyoiona ndani na nje ya soko hili hairidhishi. Nia ya Serikali ni kusaidia wafanyabiashara wadogo naona kama usaidizi wa wafanyabiashara wadogo haupo kuna utengenezaji faida kwa uongozi wa soko.”

 

“Hata mipango ya uingizaji bidhaa haimpi nafuu mfanyabiashara mdogo. Maamuzi yangu ni kwamba tutafanya tena tathmini ya uendeshaji wa soko ili tuone iwapo liendeshwe na uongozi uliopo au lichukuliwe na Jiji.”

 

“Nimeona bidhaa zilizoko ndani ni vurugu, huoni bidhaa gani ipo wapi, unamkuta anayeuza cherehani yupo katikati na muuza dawa za kilimo na panya, soko haliko vizuri, Serikali tunaenda kukaa na kufanya tathmini ya soko.”

 

“Nimuagize Waziri wa TAMISEMI kuusimamisha kazi kidogo uongozi wa Soko la Kariakoo, niwatake vyombo vya Serikali vifanye uchunguzi kwanza hal;afu tutakuja kutoa maamuzi. Kwa ujumla hali iliyopo hapa haijaniridhisha.” – amesema Rais Samia Suluhu, ziarani Kariakoo, Dar es Salaam.

Leave A Reply