The House of Favourite Newspapers

Rais Samia Akutana Uso kwa Uso na Askofu Gwajima – Video

0

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amekutana na Mbunge wa Kawe ambaye pia ni Askofu Mkuu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Mdhungaji Josephat Gwajima wakati Mhe. Rais aliposimama njiani katika eneo la Tegeta jijini Dar es Salaam akielekea Bagamoyo kurekodi kipindi maalum cha kutangaza utalii.

 

Hayo yamejiri leo Alhamisi, Septemba 2, 2021 ambapo Askofu Gwajima amempongeza Rais Samia kwa kazi kubwa anayoifanya huku akimuomba mambo mbalimbali katika Jimbo hilo ikiwa ni pamoja na ujenzi wa shule mpya, ujenzi wa Daraja la Chasimba, ujenzi wa barabara pamoja na zahanati.

 

Awali akimkaribisha kuzungumza Mbunge huyo, Rais Samia amempongeza Gwajima huku akikoleza kwa kibwagizo… “Gwajima oyeee! Tunachanjwa hatunajwi?…..

 

Baada ya hapo Rais Samia alijibu hoja hizo na kuahidi kujenga shule hiyo mpya ili kuondoa adha ya watoto kupata ajali barabarani wakati waikivuka kwenda shule zilizo mbali.

 

“Shule mliyoomba hapa itajengwa, nitazungumza na waziri wa TAMISEMI (Ummy Mwalimu) fedha zitakazokusanywa mwezi ujao, itoke sehemu ikajenge shule watakayosomea watoto wetu, wakimbie kuvuka mabarabara wasigongwe na gari,” amesema Rais Samia.

 

Leave A Reply