The House of Favourite Newspapers

Davido, Wizkid Ndani ya Bifu Jipya

0

Davido ni kama ame-catch hivi kwa msemo wa watoto wa mjini, hii ni baada ya tweet yake mapema leo kuonekana ikimlenga Wizkid na mashabiki zake ambao kwa sasa wanatamba mtandaoni kufuatia rapa wa Marekani DaBaby kufanya Freestyle ya wimbo wa ESSENCE.

 

Mkali huyo wa Afrobeats amekuja kwenye mtandao wa twitter na kuibua video ambayo inamuonesha Kanye West na Kwaya yake wakitumbuiza Wimbo wake (IF) ambao ulifanya vizuri kuanzia mwaka 2017. Ni kama anajaribu kuwafunga midomo na kuwakumbusha kwamba alikuwa mbele ya muda.

 

Davido ameandika “Hifadhi video hii, kwani itakuwa na maana baadaye.”

Leave A Reply