The House of Favourite Newspapers

Polisi Dar Wapiga Marufuku Uuzwaji Holela wa Silaha za Jadi

siro1-1

Kamishna wa Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam, Simon Sirro akizungumza jambo.

siro1-2 siro1-3

`…akionyesha baadhi ya silaha za jadi walizozikamata.

siro1-4…Akiendelea kuonyesha silaha hizo.

Na Denis Mtima/GP

JESHI la Polisi Kanda Maalumya Dar es Salaam, limepiga marufuku uuzwaji holela wa silaha za jadi kama vile, manati, pinde na mikuki huku likisema tayari limemkamata mtuhumiwa mmoja katika maeneo ya mataa ya Tazara, Mgoli Sakalani(39) akifanya biashara hiyo.

Akizungumza jijini Dar es Salaam, Kamishna wa Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam, Simon Sirro, alisema kuwa tabia hiyo imejengeka kwa wafanyabiashara wadogowadogo ambao wamekuwa wakiuza silaha mbalimbali zikiwemo mapanga, manati,visu na upinde pembezoni mwa barabara.

Kamanda Siroamewataka wafanyabiashara hao kuacha mara moja biashara hiyo ambayo imeshamiri sana katika Barabara ya Nyerere kwenye Mataa ya Tazara,Mataa ya Chang’ombe na Mataa ya Gerezani.

Alifafanua kuwa miongoni mwa wauzaji wa bidha hizo wengi wao siyo waaminifu kwani hutumia fursa hiyo kuwatishia watu wakiwa kwenye magari binafsi,magari ya umma na kisha kuwaibia mali mbalimbali kama vile simu za mkononi,saa,mikoba na laptop.

Kamanda huyo ametoa rai kwa wafanyabiashara hao kuifanya biashara hiyo sehemu maalumu kama madukani wakiwa na leseni ya biashara,vinginevyo atakayepatikana akifanya biashara hiyo kiholela atachukuliwa hatua za kisheria.

Katika hatua nyingine, Kamanda Sirro amesema kesho Jumamosi ni siku ya Polisi ijulikanayo kama ‘Polisi Day’ ambapo wataadhimisha siku ya familia katika Viwanja vya Leaders Club jijini Dar, huku mgeni rasmi akitarajiwa kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba.

Amesema baada ya hafla hiyo fupi, waziri huyo akiambatana na baadhi ya viongozi waandamizi wa Jeshi la Polisi Tanzania, wataelekea katika mikoa ya Kipolisi ya Kindondoni,Temeke na Ilala ambapo watatembelea Hospitaliza Mwananyamala, Amana na Temeke kushiriki kufanya usafi wa mazingira maeneo hayo.

Maandhimisho hayo ya siku ya familia pia yataambatana na burudani ya ngoma za asili,kuvuta kamba, kukimbiza kuku na muziki kutoka bendi ya polisi.

Comments are closed.