The House of Favourite Newspapers

Vigogo Watano Waliotajwa na Makonda Dawa za Kulevya, Tayari Wamekamatwa

Mamlaka ya Kuzuia na Kupamabana na Dawa za Kulevya  imesema kuwa inawashikilia na kuwahoji vigogo watano waliotajwa katika orodha ya watuhumiwa wanaojihushisha na biashara haramu ya dawa z akulevya.

Akizungumzia taarifa hiyo jana, Kamishna wa Intelijensia wa mamlaka hiyo, Fredrick Kibula alisema kuwa wanawahoji na kuwafanyia uchunguzi watuhumiwa hao kabla ya kufikishwa mahakamani.

Kamishna huyo alisema majina hayo ya watuhumiwa hao wanatoka miongoni mwa majina 97 Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda aliyomkabidhi Kamishna Mkuu, Rogers Sianga Februari 13 mwaka huu. Kuhusu kuwataja, Kamishna Kibula alisema muda muafaka ukifika watawataja ili wananchi waweze kuwafahamu.

Kuhusu majina ya watuhumiwa wengine 92, Kamishna Kibula alieleza kuwa wmekuwa wakiyafanyia kazi na kwamba hawakamati mtu hovyo, ni lazima wajiridhishe kuwa mtu huyu anastahili kukamatwa ndipo wafanye hivyo, lakini pia hawatangazi majina yao hadharani.

Kwa upande wake Kamishna Sianga alisema kuwa robo tatu (asilimia 78) ya wanawake wanaotumia dawa za kulevya ni waathirika wa UKIMWI kwa sababu ili kupata fedha  za kununua dawa hizo hulazimika kufanya ngono zembe na hivyo kupelekea maambukizo ya UKIMWI kuzidi kupanda.

Katika kupambana na dawa za kulevya, ni muhimu tukabadilisha mtazamo na kukazia katika kutoa elimu kwa jamii. Tunaamini kuwa jamii ikipata elimu hasa kuhusu madhara ya dawa ya kulevya, wataacha kutumia na pia kuuza, alisema Kamishna Sianga.

Comments are closed.