The House of Favourite Newspapers

Makonda Awatembelea Wahanga wa Mafuriko Dar (+Video)

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda akiwa mwenye kofia akioneshwa sehemu iliyopata madhara zaidi.

DAR ES SALAAM: Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam, Paul Makonda, amewatembelea wakazi wa Buguruni kwa Mnyamani waliokumbwa na mafuriko yaliyotokea jana katika maeneo mbalimbali jijini Dar Es Salaam.

Wakazi wa maeneno hayo wakijaribu kuvuka katika daraja lililosombwa na maji.

Aidha Makonda amesikiliza kero za wananchi wa maeneo hayo na kuwahoji baadhi ya maswali huku akigusia sababu zinazosababisha wakazi hao kushindwa kuhama maeneo ya mabondeni.

 

Wakazi wakimsikiliza kwa makini mkuu wa mkoa Paul Makonda

NIMEKUWEKEA NA VIDEO HAPA…

Na Hilaly Daudi/GPL

Comments are closed.