The House of Favourite Newspapers

Binti Aliyedondoka Mlangoni Akidaiwa ni Msukule, Nduguze Waibuka

0

Na ISSA MNALLY| RICHARD BUKOS| GAZETI LA UWAZI| HABARI

DAR ES SALAAM: Mwanamke aliyedondoka mlangoni kwenye nyumba ya mkazi wa Mabwepande jijini hapa na kutaka kuuawa kwa kuhisiwa kuwa ni mchawi, ndugu zake wameibuka na kumchukua.

Mwanamke huyo aliyefahamika kwa jina la Mwajabu Ndehere, mkazi wa Mabibo Makubuli jijini hapa alinusurika kuuawa na wananchi wenye hasira waliokuwa wakidai wamechoka kuwangiwa na kusababishiwa mikosi ambayo ndiyo chanzo cha hali ngumu ya maisha.

Wananchi hao wakiwa kwenye harakati za kumchoma moto ambapo walishamvalisha tairi, wasamaria wema kwa kushirikiana na polisi walifanikiwa kumuokoa. Baada ya kumuokoa, polisi hao waliwasiliana na uongozi wa serikali ya mtaa huo na kutafuta sehemu ya kumhifadhi kwa kuwa wao hawakuwa na sehemu ya kumpeleka baada ya kumuokoa.

Wakiwa wanatafakari sehemu ya kumpeleka, ndipo alijitokeza Mchungaji wa Kanisa la Hosana Ngome ya Yesu, Marko Mzole na kuomba kumchukua mwanamke huyo na kwenda kumfanyia maombi na kuishi naye mpaka watakapopatikana ndugu zake.

Mchungaji Mzole aliondoka na mwanamke huyo hadi kanisani kwake, akamkabidhi mkewe pamoja na wanawake wa kanisa hilo ambao walimfanyia maombi mpaka alipopata fahamu.

Akiwa anaendelea kufanyiwa maombi, ndugu zake walipata taarifa za mwanamke huyo kudondoka ambapo wananchi wenye hasira walitaka kumchoma moto lakini aliokolewa na kuhifadhiwa kanisani hapo.

Ndugu hao walifika kanisani hapo na kumkuta Mwajabu ambapo walisema awali alikuwa katika hali ya kutokwa na ufahamu lakini baada ya maombezi hayo walimshangaa kumuona katika hali ya ufahamu.

Ndugu hao baada ya kuona hali ya ndugu yao iko vizuri walimchukua ndugu yao kanisani hapo na kuondoka nae.

Leave A Reply