The House of Favourite Newspapers

Daladala Yagonga Treni, Yaua

0

Na MWANDISHI WETU| GAZETI LA AMANI| HABARI

Dar es Salaam: Mtu mmoja amefariki dunia baada ya kutokea ajali ya basi la abiria almaarufu daladala, lenye namba za usajili T435 DGG linalofanya safari zake kutoka Gongo la Mboto kwenda Mnazi Mmoja jijini hapa kuigonga Treni ya Pugu, Saa 11 alfajiri ya jana, Aprili 19, 2017 katika makutano ya reli na Barabara ya Nkurumah jijini Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa mashuhuda, ajali hiyo ilisababishwa na mwendokasi wa dereva ambaye alipofika relini, licha ya kuoneshwa ishara ya kusimama kupisha treni hiyo, alishindwa kulimudu gari na kusababisha aligonge treni hilo.

Taarifa zaidi zinaeleza kwamba, kati ya majeruhi 23 wa ajali hiyo, wanane wapo Hospitali ya Amana na wengine 15 wapo Hospitali ya Taifa Muhimbili (MOI), huku watatu kati yao wakiwa na hali mbaya.

 

Leave A Reply