The House of Favourite Newspapers

Droo Ndogo ya Tatu Ya Shinda Nyumba Awamu ya Pili Yasubiriwa Kwa Hamu

1
Mr Shinda Nyumba Awamu ya Pili akiweka kuponi sawa.

WASOMAJI wa magazeti ya Global Publishers, ambao wanaendelea kujikusanyia kuponi kwa ajili ya Bahati Nasibu ya Shinda Nyumba Awamu ya Pili, wanaisubiri kwa hamu droo ndogo ya tatu inayotarajiwa kufanyika Aprili 26, mwaka huu.

Katika droo hiyo zawadi za Pikipiki, seti ya televisheni, simu za kisasa na dinner set, zitamwagwa tena kwa wasomaji watakaoibuka kidedea. Droo hiyo inayoendeshwa na kampuni ya Global Publishers, wachap-ishaji wa magazeti pendwa ya Ijumaa, Risasi, Amani, Uwazi, Ijumaa Wikienda na lile la michezo nambari moja Tanzania la Championi, imeshafanya droo ndogo mbili.Wasomaji wa magazeti ya Global katika Viwanja vya CCM Mwinjuma wakijaza kuponi dakika za lala salama kabla ya kucheshwa Bahati Nasibu hiyo.

Akizungumza na Risasi Jumamosi, Msomaji Hamis Juma mkazi wa Kijitonyama, Dar alisema anatamani Aprili 26 ifike haraka kwani ana uhakika kwamba lazima apate zawadi kwani kila siku amekuwa akisoma magazeti ya Global Publishers na amefanikiwa kukata kuponi kibao. “Natamani siku hiyo ifike haraka kwa sababu nimeshakata kuponi nyingi za kutosha nab ado ninaendelea hivyo sitakosa zawadi mojawapo kati ya pikipiki na nyinginezo maana zipo nyingi,” alisema Hamis.Mashuhuda wakichanganya kuponi kabla ya kuchagua moja ya mshindi wa pikipiki.

Droo mbili za kwanza ambazo jumla ya wasomaji tisa wamejishindia zawadi mbalimbali zikiwemo pikipiki mbili, televisheni flat skrini mbili, dinner set na simu za kisasa seti mbili pia, zilifanyika katika ukumbi mkubwa wa burudani wa Dar Live huko Mbagala Zakhem na viwanja vya CCM Mwinjuma, Mwananyamala jijini Dar es Salaam.

Katika droo hiyo ndogo ya tatu, Meneja Mkuu wa Global Publishers, Abdallah Mrisho alisema zawadi kubwa itakuwa ni pikipiki, huku washindi wengine wakijitwalia simu za kisasa za mkononi aina ya smartphone, seti moja ya televisheni ‘flat screen’ na Dinner Set.

Leave A Reply