The House of Favourite Newspapers

TFF Yamfungia Haji Manara Mwaka 1 na Faini Ya Tsh Milioni 9

0
Ofisa Habari wa Klabu ya Simba, Haji Manara.

Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) imetangaza kumfungia Ofisa Habari wa Klabu ya Simba, Haji Manara kutojihusisha na soka kwa miezi 12 na kulipa faini ya shilingi milioni 9.

Maamuzi hayo yameamuliwa na TFF leo baada ya kuelezwa kuwa amekutwa na makosa matatu tofauti, ambapo katika moja ya adhabu alizotakiwa kupewa ni kufungiwa kwa muda wa miaka saba kama kanuni inavyoeleza.

Kiasi cha shilingi milioni 9 zinatokana na makosa matatu yote kwa jumla. Habari zaidi inakuja kuhusu suala hilo lakini imeelezwa kuwa haki ya kukata rufaa ipo wazi.

Leave A Reply