The House of Favourite Newspapers

Yanga Yaamua Kujichimbia Mazima Geita

0
Kikosi cha timu ya Yanga.

Wilbert Molandi | Championi Jumamosi | Mwanza

YANGA imeonekana kuvutiwa na kambi ya mkoani Geita, hivyo haitarejea jijini Dar es Salaam baada ya mechi dhidi ya Mbao FC, badala yake itabaki huko kujiandaa na mechi dhidi ya Prisons.
Yanga juzi Alhamisi jioni ilipanda ndege kuifuata Mbao watakayocheza nayo kesho Jumapili kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza mechi ya nusu fainali ya Kombe la FA.


Tofauti na matarajio ya wengi, Yanga moja kwa moja ikaelekea Geita kuweka kambi ya muda kabla ya kwenda Mwanza leo tayari kwa mchezo huo wa kesho.

Meneja wa Yanga, Hafidh Saleh, aliliambia Championi Jumamosi kuwa, wanadhani Geita ni mahali pazuri kwao hivyo watabaki huko kwa kambi ya siku chache hadi Mei 4, mwaka huu watakaporejea Dar es Salaam.
Hafidh alisema; “Tunacheza mechi ya ligi kuu na Prisons Mei 6, mwaka huu jijini Dar es Salaam, tumeona
ni vyema tuendelee na kambi ya Geita baada ya mechi na Mbao ili tujiandae na mchezo ujao.”


“Awali tulipanga kuweka kambi nje ya Dar es Salaam kujiandaa na mechi dhidi ya Prisons, lakini sasa tumevutiwa na kambi ya Geita hivyo tutabaki huku.”
Baada ya leo Yanga kwenda Mwanza ili icheze na Mbao kesho, timu itarejea tena Geita baada ya mchezo huo na itakaa hadi Mei 4, mwaka huu itakaporejea Dar es Salaam kwa mechi na Prisons.

Leave A Reply