The House of Favourite Newspapers

Kidoa Adaiwa Kumrithi Masogange Kwa Rammy

0

 

Msanii wa Filamu Bongo, Asha Salum ‘Kidoa’.

NA MAYASA MARIWATA | AMANI | TAMU TATU

MH! YETU MACHO! Msanii wa Filamu Bongo, Asha Salum ‘Kidoa’ sasa anadaiwa kujiweka kimapenzi kwa staa wa filamu, Rammy Gallis ambaye waliwahi kuripotiwa kutoka na Video Queen, Agnes Masogange.

Rammy Gallis akiwa na Video Queen, Agnes Masogange.

 

Mtoa ubuyu wetu aliyeomba jina lake lihifadhiwe aliweka wazi kuwa, Kidoa na Rammy wamekuwa wakionekana maeneomaeneo, mazingira yanayoonesha kuwa, wame-fall in love.

“Nyie wafuatilieni tu mtajua ukweli wa hiki ninachokisema, kuna picha f’lani zinatembea mtandaoni wakiwa kitandani, ile inaweza kuwa ni filamu lakini mbali na hilo, hawa watakuwa wanatoka maana kuna siku siyo za shooting lakini wako pamoja,” kilimwaga ubuyu chanzo hicho.

Katika kupata ukweli, mwandishi wetu alimtafuta Kidoa ambapo alipoulizwa juu ya kumrithi Masogange, alijibu kwa kifupi: “Jamani mnaonaje mkaniacha na maisha yangu?”

Msikie Rammy: “Mimi na Kidoa ni marafiki wa kawaida, najua chanzo cha yote hayo, watu wameanza kuzusha yao, si unajua tena Wabongo tulivyo!”

Leave A Reply