The House of Favourite Newspapers

Q- Chillah: Nimewasamehe Walionifelisha

0
Staa wa Bongo Fleva, Abubakari Katwila ‘Q- Chillah’.

STORI: BONIPHACE NGUMIJE | UWAZI | SHOWBIZ

MWANAMUZIKI mkongwe katika gemu la Muziki wa Bongo Fleva, Abubakari Katwila ‘Q- Chillah’ amesema kuwa akiwa na miaka kumi na tano (15) kwa sasa kwenye gemu la muziki amepitia mambo mengi ya kuumiza lakini hana budi kuwasamehe wote waliomfelisha.

Akipiga stori na ukurasa huu wa burudani, alipoulizwa kuwataja hao anaosema wamemfelisha kimuziki, Chillah alisema kuwa kuwasamehe pekee inatosha maana akiwataja halitakuwa jambo zuri na itakuwa ni sawa na kutowasamehe, zaidi anamuachia Mungu.

“Unajua matokeo ya mimi kuwa hapa ni baada ya kufelishwa na wadau wa muziki ambao nimekuwa nikifanyanao kazi katika nyakati tofauti, lakini nimeamua kumuachia Mungu na yeye ndiye atakayenilipia na kuniinua zaidi ya hapa nilipo kwa sasa,” alimaliza Chillah.

Leave A Reply