The House of Favourite Newspapers

Kampuni Ya Mawasiliano Ya Zantel Yajumuika Na Wafanyakazi Na Wadau Wake Kwa Futari Jijini Dar

0

1b.JPG
Baadhi ya wafanyakazi wa Zantel wakijumuika katika tafrija ya futari maalumu kwa ajili yao katika kipindi hiki cha mfungo Mtukufu wa Ramadhani. Tafrija hiyo ilifanyika jana jijini Dar es Salaam.
2.JPG Meneja Chapa na Mawasiliano wa Zantel, Rukia Mtingwa (kushoto) akitoa huduma ya chakula kwa baadhi ya wafanyakazi wa Kampuni hiyo waliojumuika na wateja na wadau mbalimbali katika tafrija ya futari iliyofanyika jana jijini Dar es Salaam.
3.JPG
Mkuu wa Kitengo cha Rasilimali Watu Zantel, Joanitha Mrengo (wa pili kushoto) akitoa huduma ya chakula kwa Mkurugenzi Mkuu wa Zantel Benoit Janin (wa kwanza kulia) katika tafrija ya futari iliyofanyika jana jijini Dar es Salaam. Tafrija hiyo ilikuwa ni mahususi kwa ajili ya wafanyakazi na wadau wa kampuni hiyo. Anayeshuhudia (kushoto) ni Afisa wa Kitengo cha Rasilimali watu Zantel, Maryam Khatri.
5.JPG
Afisa wa Kitengo cha Rasilimali watu Zantel, Maryam Khatri (kushoto) akitoa huduma ya chakula kwa wafanyakazi wa Zantel katika tafrija ya futari iliyofanyika jana jijini Dar es Salaam. Tafrija hiyo ilikuwa ni mahususi kwa ajili ya wafanyakazi na wadau wa kampuni hiyo.
6.JPG
Baadhi ya wafanyakazi wa Zantel wakijumuika kupata futari katika tafrija iliyoandaliwa na Kampuni hiyo katika kipindi hiki cha mfungo Mtukufu wa Ramadhani ambayo ilifanyika jana jijini Dar es Salaam.
7.JPG
Mkurugenzi Mkuu wa Zantel, Benoit Janin akizungumza wakati wa tafrija ya futari maalumu iliyoandaliwa na Kampuni hiyo kwa ajili ya wafanyakazi na wadau mbalimbali katika kipindi hiki cha mfungo Mtukufu wa Ramadhani. Tafrija hiyo ilifanyika jana jijini Dar es Salaam.

Leave A Reply