The House of Favourite Newspapers

Jay Z Aonekana Nje kwa Mara ya Kwanza

0

Jay Z akitoka hospitalini huku akitabasamu.

LABDA hukuipata! Ishu ipo hivi! Kwa mara ya kwanza mwanamuziki mwenye jina kubwa katika tasnia ya Muziki wa Rap nchini Marekani, Jay Z ameonekana nje huku akitabasamu baada ya mkewe, Beyonce kujifungua mapacha wawili, wa kiume na kike wiki iliyopita.

Staa huyo anayeshika nafasi ya tatu kwa wanamuziki wenye mkwanja mrefu wa dola milioni 610 ambazo ni zaidi ya shilingi trilioni 1.3, hakutoka nje tangu mkewe huyo ambaye pia ni mwanamuziki ajifungue watoto hao.

Ikumbukwe kuwa kabla ya kupata watoto hao, tayari yeye na mke wake, Beyonce walikuwa na mtoto mmoja aitwaye Blue Ivy ambaye alizaliwa mwaka 2012 ambapo kwa sasa ana miaka 5.

Leave A Reply