The House of Favourite Newspapers

J LO Kufunga Ndoa kwa Mara ya Nne

0

 

MWANAMAMA kutoka Marekani, Jennifer Lopez maarufu kama J Lo, yuko mbioni kufunga ndoa kwa mara ya nne maishani mwake, baada ya hivi karibuni kuvalishwa pete ya uchumba na mpenzi wake wa sasa, anayefahamika kwa jina la Alex Rodriguez.

Tukio hilo la kuvalishwa pete lilifanyika nchini Ufaransa walikokwenda kwa ajili ya mapumziko na mipango yao ni kwamba shughuli hiyo ya harusi, itagharimu zaidi ya dola milioni 3.

 

Chakula na vinywaji peke yake vitagharimu dola 500,000 na baada ya msosi wageni waalikwa watapata burudani ya maonyesho ya jinsi ya kucheza na moto ambayo yanagharimu dola 150,000. Gharama nyingine ni pamoja na mavazi ya maharusi hao pamoja na watoto wa Jennifer Lopez.

Na: Isri Mohamed, (GPL)

Leave A Reply