The House of Favourite Newspapers

Tambwe Amwaga Wino Kuitumikia Yanga Miaka 2

0

 

Mshambuliaji Amissi Tambwe amesaini mkataba wa miaka mwili wa kuendelea kuichezea Yanga.

Uamuzi wa Tambwe kusaini mkataba huo ni habari njema kwa mashabiki na wapenzi wa Yanga ambao walikuwa na wasiwasi kwa nyota huyo kuondoka msimu huu baada ya kumalizika kwa mkataba wake.

 

 

Uamuzi wa Tambwe umekuja siku mbili baada ya mshambuliaji Donald Ngoma  kusaini mkataba wa miaka mwili na kuzidi kuimalisha safu ya ushambuliaji wa mabingwa hao wa Ligi Kuu Bara.

Tangu alipojiunga na Yanga akitokea Simba, Tambwe amekuwa na mchango mkubwa kwa timu hiyo akiwezesha kutwaa mataji mawili ya Ligi Kuu Bara pamoja na kufuzu kwa hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika.

Leave A Reply