The House of Favourite Newspapers

Pluijm: Hakuna Wa Kuisumbua Singida United

0
Kocha Mkuu wa Singida United, Hans van Der Pluijm.

SINGIDA United ipo jijini Mwanza kwa maandalizi ya msimu ujao wa Ligi Kuu Bara ambapo tayari kocha wake, Hans van Der Pluijm amesema hakuna timu itakayowasumbua katika ligi hiyo.

Akizungumza na Championi Jumatano, Pluijm raia wa Uholanzi, amesema atahakikisha timu yake inakuwa mfano wa kuigwa kwa timu

zilizopanda daraja na kufanya vizuri nchini. “Tupo katika maandalizi kabambe na kimsingi nataka Singida iwe timu ya mfano na kutokana na maandalizi ninayofanya sijaona timu ya kunisumbua katika msimu ujao,” alisema Pluijm.

Pluijm aliyewahi kuwa kocha wa Yanga, amesisitiza kuwa licha ya timu yake kupanda daraja watu wasiidharau kwani itawashangaza kwa kufanya vizuri katika mechi zake.

“Najua wapo baadhi ya viongozi watatudharau kwa kuwa sisi ni wageni katika ligi, mimi niseme kwamba tuko vizuri zaidi ya wanavyofikiria kwani kwa sasa nafanya kazi ya kuingiza mfumo wangu kikosini,” alisema Pluijm

Johnson James | Championi Jumatano

Leave A Reply