The House of Favourite Newspapers

Sirro Amteua kamanda Mpinga Kuwa RPC wa Mbeya

0
Kamanda Mpinga.

 

Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP SAIMON SIRRO, amefanya mabadiliko ya Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani pamoja na Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mbeya.

 

Katika mabadiliko hayo, aliyekuwa Kamanda wa Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani, MOHAMED MPINGA anakuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya,na nafasi yake inachukuliwa na Bwana FORTUNATUS MUSILIM.

 

Taarifa ya Jeshi la Polisi kwa vyombo vya Habari zinasena aliyekuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Bwana   DHAHIRI KIDAVASHARI amehamishiwa Makao Makuu ya Upelelezi.

 

Uhamisho huo ni wa kawaida katika kuboresha utendaji wa kazi za Polisi kwa mujibu wa kanuni, taratibu na miongozo ya Jeshi la Polisi.

Leave A Reply