The House of Favourite Newspapers

Pluijm: Najua Singida United Tunadharaulika Ila Watatukoma

0
Kocha Mkuu wa Singida United, Mholanzi Hans Van Der Plujm.

KUELEKEA Ligi Kuu Bara msimu ujao, Kocha Mkuu wa Singida United, Mholanzi Hans Van Der Plujm amesema anafahamu wanadharaulika lakini ametamba kikosi chake kutoa ushindani mkubwa mbele ya vigogo Simba na Yanga.

Akizungumza na Championi Jumamosi, Pluijm alisema kuwa yeye anaiandaa timu yake kushindana katika ligi na kuleta ushindani na lengo lake ni kuhakikisha anafanya vyema kwenye msimu wake wa kwanza akiwa na kikosi hicho.

Wachezaji wa Singida United wakifanya mazoezi.

“Kutokana na jinsi ninavyoiandaa timu yangu malengo yangu ni kuifanya Singida United ilete changamoto kwenye ligi na siyo kushiriki kama ambavyo wengi wanafikiria. “Najua tunadharaulika baada ya kupanda daraja lakini mimi niseme kwamba tutaleta ushindani mkali sana na malengo yetu ni kushika nafasi za juu kwenye msimamo wa ligi,” alisema Pluijm.

Leave A Reply