The House of Favourite Newspapers

Zidane Alia Na Morata Kuondoka Agoma

0
Kocha wa Real Madrid, Zinedine Zidane.

KOCHA wa Real Madrid, Zinedine Zidane amesema timu yake ina uhaba wa washambuliaji baada ya kumuuza Alvaro Morata kwenda Chelsea.

Kocha huyo amesema kuwa washam­buliaji waliopo kwenye timu hiyo hawatoshi, huku akisisitiza kuwa mshambuliaji bora wa timu hiyo Cristiano Ronaldo, atabaki kwenye kikosi hicho..

Morata ambaye alikuwa akiwindwa kwa nguvu kubwa na Manchester United aliuzwa kwenye kikosi cha Chelsea kwa kitita cha pauni milioni 60, zaidi ya shilingi bilioni 171.

Hata hivyo, bado timu hiyo inamwinda staa wa Monaco, Kylian Mbappe, ambaye anaweza kumaliza tatizo hilo kwenye timu hiyo.

“Alvaro ameondoka na sasa tuna tatizo kubwa la washambuliaji kwenye timu yetu.

Aliyekuwa mshambuliaji wa Real Madrid, Alvaro Morata.

 

“Nafikiri kila mmoja aliona jinsi alivyocheza msimu uliopita, al­ionyesha kiwango cha hali ya juu sana  na hakika tulitaki­wa kuwa naye msimu huu.

“Tutajaribu kuona ni kitu gani tunaweza kufanya kabla usajili huu hau­jafungwa lakini naamini kuwa tutamaliza vi­zuri,” alisema kocha huyo raia wa Ufaransa.

Alipoulizwa kuwa taarifa kuwa anataka kumsajili, Mbappe kutoka Monaco, alisema: “Ni jambo ambalo limejadiliwa klabuni, lakini siwezi kuzungumza sana kwa kuwa tunajadili wachezaji ambao wapo nasi kwa sasa hawa ndiyo tupo nao kwenye timu hii.”

Zidane ni kati ya makocha waliofanikiwa kwa muda mfupi akiwa amefanikiwa kutwaa ubingwa wa Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa mi­simu miwili mfululizo, lakini pia msimu ulio­pita alifanikiwa kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya Hispania, La Liga.

FULL VIDEO; Mapambano Ngumi za Global TV – Ubingwa wa Afrika Mashariki na Kati, Tanzania Bingwa

Leave A Reply