The House of Favourite Newspapers

Dallas Wamtwaa Dirk Nowitzki

0
Staa Dirk Nowitzki.

TIMU ya Dallas Mavericks imetangaza kumsajili staa Dirk Nowitzki kwa ajili ya msimu ujao wa Ligi Kuu ya NBA.

Hata hivyo, timu hiyo bado haijaweka wazi kuwa imemsajili mchezaji huyo kwa kitita kikubwa kiasi gani hadi sasa pamoja na kwamba wamekiri kuwa dili hilo limekamilika.

 

Nowitzki anarejea kwenye NBA kwa msimu wake wa 20 akiwa anaungana na mastaa wengine kama Kobe Bryant ambao walicheza ligi hiyo kwa muda mrefu.

 

Wakati akicheza msimu wa 19, alikuwa na timu ya Dallas ambapo Nowitzki alifanikiwa kuonyesha kiwango cha hali ya juu kuliko kipindi kingine chochote kile ambacho aliwahi kucheza ligi hiyo.

 

Hata hivyo, mwaka wake wa mafanikio makubwa ni msimu wa 2002-03, ambapo alifanikiwa kutwaa ubingwa wa NBA. Pia alifanikiwa kuiongoza Mavericks kucheza michezo ya mtoano mara 15 kuanzia mwaka 2001 hadi 2016.

 

Nowitzki, hadi sasa ameshafunga pointi 30,260 kwa kipindi chake chote alichocheza kwenye NBA na inaaminika kuwa ni kati ya wachezaji ambao msimu ujao wataonyesha kiwango cha juu sana.

Leave A Reply