The House of Favourite Newspapers

Sol Campbell Alivyosherehekea Ushindi Wa Arsenal Na Mashabiki Wa Tanzania

0
Mchezaji wa zamani wa Arsenal, Sol Campbell (katikati) akiwa na mashabiki wa Arsenal baada ya mechi ya Arsenal dhidi ya Chelsea kwenye Viwanja vya Leaders Club jijini Dar . Mabingwa wa Kombe la FA, Arsenal wametwaa Ngao ya Jamii kwa kuifunga Chelsea kwa penalti 4-1 baada ya kutoka sare ya bao 1-1 katika dakika 90.
…Wakishangilia na Mr SportPesa.
 Sol Campbell akiangalia mechi hiyo
…Mechi ikiendelea.
…Akiendelea kuangalia mechi hiyo.
Muonekano wa screen iliyofungwa uwanjani hapo.
Wadau mbalimbali wakiendelea kuangalia mechi hiyo.
Mashabiki wa Arsenal wakiwa na shangwe baada ya ushindi.
…Wakiendelea kupongezana

Mchezaji wa zamani wa Arsenal, Sol Campbell, leo aliiangalia mechi ya timu yake hiyo ya zamani ilipokuwa ikimenyana na Chelsea katika mchezo wa kugombea Ngao ya Jamii.

Mchezaji huyo aliuangalia mpambano huo kupitia luninga kubwa kwenye Viwanja vya Leaders Club jijini Dar sambamba na umati mkubwa wa mashabikii wa timu hiyo hapa nchini. Ulipofika wakati wa mapumziko, mchezaji huyo aliwapa zawadi mashabiki aliowauliza maswali kuhusu historia yake ya soka na kumjibu vizuri.

PICHA : RICHARD BUKOS / GPL

Leave A Reply