The House of Favourite Newspapers

GLOBAL TV YAANZISHA KAMPENI ‘SAIDIA JINI KABULA’

0
global tv saidia jini kabula
Jini Kabula

KITUO cha televisheni namba moja ya mtandaoni ya Global TV Online kwa kushirikiana na ndugu na wadau, imeanzisha kampeni maalum ya kuchangia gharama za kusaidia matibabu ya mwigizaji wa sinema za Kibongo, Miriam Jolwa ‘Jini Kabula’ anayeumwa ugonjwa unaotajwa kuwa wa matatizo ya afya ya akili.

 

Mratibu wa kampeni hiyo iliyopewa jina la ‘Support Jini Kabula For Treatment’, Isri Mohamed aliliambia Ijumaa Wikienda kuwa, lengo la kuanzisha kampeni hiyo ni kutokana na kuguswa na tatizo la Jini Kabula ambaye hivi karibuni alifika ofisi za Global Publishers akihitaji msaada hivyo kuona ni vyema Watanzania wakajitolea kuchangia gharama za matibabu.

 

Isri alisema kuwa, mara baada ya Global TV kupata wazo hilo, waliwasiliana na ndugu wa Jini Kabula, ambao kwa pamoja walikubaliana kufanyika kampeni hiyo.

 

“Sisi kama Global TV Online tumeguswa na tatizo la Jini Kabula, ndiyo maana tunawaomba, wasanii wenzake, marafiki, jamaa na Watanzania wote kwa pamoja tumchangie mwenzetu gharama za matibabu kwani ni Mtanzania mwenzetu na anahitaji matibabu ili arudi kwenye hali yake ya kawaida.

 

“Tunawaomba kwa yeyote anayeguswa ajitolee kwa chochote kusaidia matibabu ya Jini Kabula, kuanzia leo Jumatatu, Agosti 7, 2017. Matatizo humkumba kila mtu, hata yeye hakufahamu kama angekumbwa na ugonjwa kama huo, chonde chonde Watanzania tumsaidie Jini Kabula atibiwe apone arudi kuwa mwenye furaha kama mwanzo,” alisema Isri.

 

Naye kaka wa Jini Kabula, Dustan Jolwa kwa niaba ya ndugu alishukuru Global Tv kwa hilo na kuwaomba watanzania na wasio watanzania wajitokeze kumsaidia dada yake.

Namba ya simu ambayo inatumika kukusanya michango hiyo ni; 0712565369 ambayo ni ya dada wa Jini Kabula aitwaye, Daynes Jolwa.

Stori: Brighton Masalu | IJUMAA WIKIENDA

=====

Exclusive: Maskini Jini Kabula! Ukimsikia Utalia, Anatia Huruma

Leave A Reply