The House of Favourite Newspapers

Lissu Apanda Kortini Kesi ya ‘Dikteta Uchwara’

0
Tundu Antipas Lissu.

MBUNGE wa Singida Mashariki na Rais wa Chama cha Mawakili Tanganyika (TLS), Tundu Antipas Lissu leo Septemba 4, 2017 amefika katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kwenye kesi ya ‘Dikteta Uchwara’ inayomkabili.

Lissu baada ya kuwasili mahakamani hapo, upande wa mashtaka umeieleza mahakamahiyo kuwa imefunga ushahidi katika kesi ya hiyo.

Wakili wa serikali, Mutalemwa Kishenyi amemueleza Hakimu Mkazi Mkuu, Godfrey Mwambapa kuwa kesi hiyo imeitishwa kwa ajili ya ushahidi lakini wamemaliza ushahidi, ambapo Lissu alisema wakili wake Peter Kibatala hakuwepo mahakamani, isipokuwa aliwasilisha hoja kwamba hana kesi ya kujibu.

Hata hivyo, wakili Kishenyi alidai kuwa hakuna kipengele kinachoruhusu mshtakiwa kusema hana kesi ya kujibu ama la. Kutokana na hatua hiyo, Lissu amedai kuwa hoja za upande wa mashtaka sio sahihi, kwa sababu kifungu cha 230 cha Mwenendo wa Makosa ya Jinai kinatoa nafasi kueleza kama kuna kesi ya kujibu ama la.

“Hivyo tunaomba tupate fursa kwamba kwa ushahidi uliopo katika rekodi hakuna kesi ya kujibu,”.

Hata hivyo, wakili Kishenyi alidai kuwa anasisitiza kwamba hakuna kifungu cha namna hiyo, hivyo mahakama itoe uamuzi kama ana kesi ya kujibu ama la.

Kutokana na mvutano huo, Hakimu Mwambapa amesema anakubaliana na hoja za upande wa mashtaka kwamba hakuna kifungu kinachomruhusu mshtakiwa kueleza kama ana kesi ya kujibu ama la, isipokuwa ana haki ya kuieleza mahakama.

Hakimu Mwambapa amesema anatoa siku 14 kwa pande zote mbili kuwasilisha hoja zao September 18/2017 na October 4/2017 atatoa uamuzi kama mshtakiwa ana kesi ya kujibu au hakuna.

Katika kesi hiyo Lissu ambaye pia ni Mnadhimu wa Kambi ya Upinzani Bungeni na Mwanasheria wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) anadaiwa kutoa kauli za uchochezi dhidi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano.

 

Leave A Reply