Wafanyakazi Kampuni ya China ya Anhui Dar Wagoma

kampuni ya China

Wafanyakazi hao wakiwa nje ya jengo wanalojenga wakiwa wamegoma.

kampuni ya China

Askari waliofika hapo kwa ajili ya kulinda usalama.

kampuni ya China

WAFANYAKAZI wa kampuni ya China ya Anhui Foreign Economic Construction Group Co. Ltd wanaojenga jengo moja mkabala na Ukumbi wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam, leo walijazana nje ya jengo hilo wakishinikiza kupewa mikataba ya ajira ya kudumu.

Mmoja wa wafanyakazi hao alipotakiwa na mtandao huu kueleza kisa cha kuwa nje badala ya kuwa ndani wakichapa kazi, alisema walitoka nje wakiwa wamegoma ili kushinikiza kupewa mikataba ya kudumu na kuongezewa posho za kila siku.

Walitaka posho hiyo iongozwe kutoka sh. 10,000 kwa siku hadi 12,000.

Mtandao huu uliutafuta uongozi unaohusika na ujenzi huo lakini haukuweza kuonana nao kwa madai kuwa wahusika walikuwa wamekwenda kuonana na uongozi wa serikali ili kushughulikia tatizo hilo.

 

NA DENIS MTIMA/GPL

Loading...

Toa comment