Msanii chipukizi, Hamorapa, jana alikonga nyoyo za mashabiki wa muziki wa kileo alipoungana na wasanii wengine katika tamasha la Full Dozi lililofanyika ukumbi wa Dar Live Mbagala-Zakhem jijini Dar es Salaam usiku wa kuamkia leo.
Mwanamuziki huyo kijana aliwaweka mashabiki wake ‘roho juu’ kwa ubunifu wake mkubwa akiwa stejini ambapo aliweza kucheza na kuimba kwa wakati mmoja.