Hamorapa Ang’arisha Nyota Yake Tamasha la Full Dozi

Msanii anayekuja kwa kasi, Hamorapa, akiwanyanyua mashabiki kwenye tamashala Full Dozi lililofanyika Ukumbi wa Taifa wa Burudani wa Dar Live jijini Dar es Salaam usiku wa kuamkia leo.

…Akiongea na mashabiki hao kwa aina yake.

Mashabiki wakiwa ‘wamechanguliwa’ na manjonjo ya Hamorapa.

Msanii chipukizi, Hamorapa, jana alikonga nyoyo za mashabiki wa muziki wa kileo alipoungana na wasanii wengine katika tamasha la Full Dozi lililofanyika ukumbi wa Dar Live  Mbagala-Zakhem  jijini Dar es Salaam usiku wa kuamkia leo.

Mwanamuziki huyo kijana aliwaweka mashabiki wake ‘roho juu’ kwa ubunifu wake mkubwa akiwa stejini ambapo aliweza kucheza na kuimba kwa wakati mmoja.

Toa comment