The House of Favourite Newspapers

GWAJIMA ALIAMSHA DUDE KWA MBWEMBWE KUPIGWA RISASI KWA LISSU! (VIDEO)

0
Askofu wa Kanisa la Glory Of Christ Tanzania Church (GCTC) ‘Ufufuo na Uzima’, Dk. Josephat Gwajima ‘Mzee.

 

ASKOFU wa Kanisa la Glory Of Christ Tanzania Church (GCTC) ‘Ufufuo na Uzima’, Dk. Josephat Gwajima ‘Mzee wa Dude’ ameomba kupewa muda ili ajiridhishe kabla ya kuwaanika kwa majina watu wanaoitwa… “wasiojulikana…” walimpiga risasi na kumjeruhi vibaya Mbunge wa Singida Mashariki na Mwanasheria Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Wakili Tundu Antipas Augustino Mgwai Lissu ‘TL’ kiwa ni moja ya kutimiza majukumu yake ya ki-askofu kwa kuwa hakuwa nchini kwa zaidi ya siku 80, Ijumaa Wikienda lilikuwepo.

Usipitwe na Matukio, Install ===>Global Publishers App

Katika mahubiri yake yaliyofurika umati mkubwa jana huku akichombeza kwa mbwembwe na mikogo ya kijasiri, Gwajima ambaye siku za hivi karibuni amejizolea umaarufu mkubwa kutokana na tabia yake ya kuweka hadharani mambo mazito bila kujali cheo na nafasi ya mtu, alikemea vibaya kitendo hicho na kuogeza kuwa waliomwaga damu ya Lissu itawalilia na kisasi dhidi yao kiko mikononi mwa Mungu.

…Akiongea neno

“Damu ya kiumbe hai ina sauti na kilio, maandiko matakatifu yanathibitisha hilo kupitia Biblia katika vitabu mbalimbali, nakuhakikishieni wale wote waliomwaga damu ya Tundu Lissu ni lazima itawarudia, ni lazima tukemee maovu haya kwani nchi yetu imejaa amani na utulivu hivyo hatuko tayari kuona watu wachache wanajaribu kutuchafulia.

“Ndugu zangu risasi ni kitu kibaya mno, inahitaji mtu mwenye ujasiri wa ajabu tu kukamata bunduki na kumfyatulia binadamu mwenzako na kwa kweli tukio la Tundu Lissu kupigwa risasi limetia doa kubwa mno na nataka niseme wazi kwamba nipeni muda na nitabaini na kuwaweka hadharani watu hao, nitawataja maana sikuwepo nchini hivyo naona kama nguvu na mtandao wangu vinalegalega, namuombea Tundu Lissu arejewe na afya yake na ataopona kwa Jina la Yesu,” alisema Dk. Gwajima.

Naye kwa upande wake, mdogo wa Tundu Lissu, Vincent Mgwai Lissu  aliwatia simanzi waaumini waliohudhuria kanisani hapo kwa kueleza namna ambavyo kaka yake alikuwa akifuatiliwa kwa muda mrefu na waru wasiojulikana na kwamba hatimaye wametimiza matakwa ya mioyo yao, jambo ambalo linapaswa kukemewa kwa nguvu zote na kutumia nafasi hiyo kuwashukuru waumini na Wanzania kwa ujuma kwa kuguswa na kumombea kaka yake bila kujali tofauti za kiitakadi na vyama.

“Kaka yangu amemwaga damu nyingi, lakini siku kadhaa nyuma kabla ya tukio la kupigwa kwake risasi, alitueleza kama wanafamilia juu ya ufuatiliwaji aliokuwa akifanyiwa na watu wasiojukana na kuanika ukweli huo kwa vyombo vya habario, asantani kwa kumuombea na hakika sisi kama wanafamilia ya Lissu, tumeuona umoja wa Watanzania,” alisema Vincent Lissu.

Mbunge wa Ubungo (Chadema), Saed Kubenea aliwasihi Watanzania kuzidi kuungana pamoja kwa kukemea na kulaani juu ya tukio hilo baya.

Habari: Brighton Masalu/GPL

Usipitwe na Matukio, Install ===>Global Publishers App

 

Leave A Reply