The House of Favourite Newspapers

Maxime: Upepo Umenibadilikia Kagera

0
Kocha wa Kagera Sugar, Mecky Maxime.

MECKY Maxime ni miongoni mwa makocha bora wazawa, wanaofundisha timu za Ligi Kuu Bara akiwa na mafanikio makubwa tangu alipokuwa katika timu ya Mtibwa Sugar misimu kadhaa iliyopita ambapo alikuwa akiifikisha katika nafasi nzuri ya msimamo wa ligi kabla ya kuachana nayo katika msimu wa 2015/16.

 

Maxime ameanza kuinoa Kagera Sugar msimu uliopita ambapo alifanikiwa kumaliza ligi katika nafasi ya tatu ya msimamo wa ligi huku akiteuliwa kuwa kocha bora wa msimu. Msimu huu mambo yameonekana kumuendea kombo baada ya mechi sita kutoshinda hata moja, akiwa amepoteza nne na kujikuta mkiani mwa msimamo wa ligi hiyo.

Kati ya mechi sita aliyocheza, amefanikiwa kutoa sare michezo miwili na kupoteza michezo minne, hivyo kujikuta akijikusanyia pointi mbili tu. Championi Jumatatu limefanya mazungumzo na Maxime ili kubaini nini tatizo, kufuatia matokeo hayo mabaya aliyoyapata mwanzoni mwa msimu.

 

UNAZUNGUMZIAJE LIGI?

“Ligi ni ngumu, kila timu tunayokutana nayo inaonyesha ushindani wa hali ya juu, na ndiyo maana hadi sasa hatujapata matokeo hata mchezo mmoja. “Nimejipanga kuona nafanikiwa kufanya vyema katika michezo inayofuata, naamini ligi bado na tutajipanga na kuwa vizuri ili kurejea katika kiwango chetu cha kawaida, ili tukae katika nafasi nzuri ya msimamo wa ligi. “Kila timu inaonyesha bidii tofauti na ilivyokuwa msimu uliopita, hivyo kusababisha ligi kuwa na upinzani mkubwa.

 

NINI TATIZO LA KUFANYA VIBAYA TIMU YAKO?

 

“Kilichotokea kwa upande wetu ni upepo tu kwani hakuna tatizo lolote linalonikabili, msimu h u u n a o n a umetuj i a vibaya tu. “Hali hii naichukulia kama misukosuko tu ambayo imetukuta na ni ya kawaida ambayo hata katika maisha yapo. “Watu wanadhani tulivyoanza msimu uliopita ndio tungeanza

m s i m u h u u , m a m b o yanabadilika kwani kuna ushi n d a n i mkubwa, lakini naamini haya yote ni mapito na yatapita tu ili kuweza kukaa sawa na kufanya vyema katika mechi zijazo, ligi ndiyo kwanza ipo mwanzo.

 

JE, KUNA T A T I Z O NDANI YA UONGOZI? “Sina tatizo lolote dhidi ya viongozi wala wachezaji kwa kuwa na madai yoyote, isipokuwa mambo ya kimpira tu. “Ninachohitaji hivi sasa ni kukipanga  kikosi changu kiweze kuimarika kwa

kufanyia kazi upungufu uliojitokeza ili kuwa na kikosi imara.

VIPI TIMU YAKO UNAIONAJE? “Kikosi c h a n g u kwa ujumla siyo k i b a y a , w a c h e zaji wanajituma kama inavyotakiwa ila bahati siyo yetu, nitafanyia kazi baadhi ya vitu vidogovidogo vinavyojitokeza katika kila m c h e z o , naamini tutakaa sawa. “ I w a p o timu ing e k u w a mbovu au ina upu n g u f u wowote, ningeachana nayo

mapema lakini naamini tutakuja kufanya vizuri tu huko mbele, nakiamini kikosi changu.

 

VIPI KUHUSU PENGO LA MBA-RAKA YUSUPH?

“Kwa upande wangu hakuna pengo la mshambuliaji Mbaraka Yusuph katika kikosi changu, washambuliaji waliopo wanao uwezo wa kuziba pengo lake, naamini muda haujafika, ukifika watafunga tu.

USHINDANI UNAUZUNGUMZIAJE? “Ushindani ni mkubwa na kila timu unayokutana nayo ni kama fainali, hivyo  kikubwa ni kujipanga na kujituma ili kufanya vizuri.

 

V I P I KUHUSU UKOCHA B O R A MSIMU HUU?

“Kuhusu ukocha bora kwa sasa bado sana, k w a n i ligi ndiyo kwanza ipo katika hatua za awali, u n a w e z a k u s h a n g a a namaliza ligi nikiwa bingwa au nafasi ya pili. “Hakuna kocha anayeweza kujihakikishia kutwaa ukocha bora kwa kipindi hiki, kwani lolote linaweza kutokea, tusubiri ligi iishe, hata kwa upande wangu sijakata tamaa, naamini nitafanya vizuri.

VIPI KUHUSU WACHEZAJI WAKONGWE W A N A K U SAIDIA? “Wachezaji wakongwe kwa upande wangu wana msaada mkubwa kutokana na uzoefu wao kwenye ligi, mambo bado hayajakaa sawa, yakikaa sawa mtaipenda Kagera.”

MAKALA: KHADIJA MNGWA, CHAMPIONI JUMATATU

Leave A Reply