The House of Favourite Newspapers

Bifu Zito Conte vs Mourinho, Warushiana Maneno

0
Kocha Jose Mourinho wa Manchester United

VITA ya maneno baina ya makocha wakubwa wa timu mbili Chelsea na Manchester United inazidi kukolea, ambapo sasa kuna moto mpya umewashwa.

Kocha Jose Mourinho wa Manchester United ndiye aliyeanza kumtupia madongo wenzake, Antonio Conte wa Chelsea kuwa anapenda kulialia akidai wachezaji wake ni majeruhi.

 

Kauli hiyo ikaonekana kumchoma kwenye moyo Conte ambaye naye akamjia juu mpinzani wake huyo ikiwa ni wiki chache kabla ya timu za makocha hao hazijakutana kwenye Premier League.

 

“Kama ananizungumzia mimi nafikiri anatakiwa kufikiria kuhusu timu yake, hatakiwi kuanza kufikiria wengine,” kauli hiyo aliitoa Conte baada ya timu yake kupata sare ya mabao 3-3 dhidi ya Roma, usiku wa kuamkia jana licha ya kuwa Chelsea iliongoza kwa mabao 2-0 katika mchezo huo.

 

“Nadhani muda mwingi Mourinho huwa anafikiria nini kinachoendelea Chelsea, ilikuwa hivyo pia hata msimu uliopita, afikirie kuhusu timu yake aachane na sisi.”

Kocha wa Chelsea, Antonio Conte

Mourinho ambaye timu yake ilishinda bao 1-0 dhidi ya Benfica, usiku wa kuamkia jana alinukuliwa akisema: “Huwa sizungumzi kuhusu wachezaji majeruhi, kuna makocha wengine kazi yao ni kulia, kulialia, mimi siliilii, ninawaweka pembeni wale ambao sipo nao na ninafanya kazi na waliopo.

 

“Nikiamua kulia hapa ninaweza kufanya hivyo kwa dakika tano. Hatuna Zlatan, Pogba, Fellaini, Marcos Rojo. Tulienda Liverpool tukiwa na viungo wawili tu na sikulia.

 

“Leo (juzi) tumemchezesha mtoto Scott McTominay, kwa kuwa sikuwa na njia nyingine, tukiwa hivyo tumecheza mechi 12, tumeshinda 10 na sare mbili, sijaona tatizo

Leave A Reply