The House of Favourite Newspapers

Simba vs Yanga Ni Vita Na Kisasi Uwanja wa Uhuru Kesho

0
Wachezaji wa timu ya Yanga.

MECHI za Ligi Kuu Bara z i n a t a r a j i a kuendelea wikiendi hii kwa mzunguko wa nane kuchezwa, huku miamba miwili ya soka Tanzania, Simba na Yan­ga ikitarajia kukutana kwenye Uwanja wa Uhu­ru jijini Dar es Salaam, kesho Jumamosi.

 

Mchezo huu unatara­jiwa kuwa na ushindani wa hali ya juu kutokana na timu hizo kuwa katika nafasi sawa ya msimamo wa ligi licha ya Simba kuongoza kwa idadi ya mabao ya kufunga, huku kila moja ikihitaji kukaa kileleni.

Mechi hii inatarajiwa kuwa ni ya vita na kisasi kutokana na hali jinsi ilivyo katika mechi husika ambapo kila upande utahitaji ku­fanya vyema.

 

Yafuatayo ni baadhi ya mambo ambayo yanatarajiwa kuifanya mechi hiyo kuwa ni ya vita na kisasi.

MAKOCHA KUTETEA VIBARUA VYAO

Imekaa vibaya kwa upande wa makocha wa timu zote mbili, kutokana na historia za timu hizo ambapo mara nyingi makocha wamekuwa wakifungashiwa vi­rago vyao pale wanapofungwa na wapinzani wao.

Hivi karibuni kulizuka uzushi juu ya Yanga kutaka kumuondoa ko­cha wake, George Lwandamina kutokana na matokeo mabaya katika mechi za awali jambo am­balo uongozi wa klabu hiyo ulika­nusha, lakini waswahili husema lisemwalo lipo, hivyo mechi hiyo inaweza kuwa katika wakati mgu­mu kwa upande wake.

Kikosi cha timu ya Simba.

Vilevile kwa upande wa Simba, Kocha Joseph Omog amekalia kuti kavu kwa muda mrefu kuto­kana na uongozi wa klabu hiyo kutaka kumuondoa kutokana na madai ya kutokifundisha vyema kikosi hicho kwa kuona kuwa kimemzidi uwezo, lakini mkataba aliosaini umeonekana kumbeba kutokana na baadhi ya vipengele kuwabana waajili wake.

 

Hivyo basi, mechi hii ndiyo itakayotoa maamuzi juu ya kuen­delea kuwepo katika kikosi hicho kwa kuwa inadaiwa kuna kipenge­le alichosaini kinaeleza kuwa iwapo t i m u haitaongoza msimamo wa ligi, itawapa nguvu viongozi kuweza kuvunja kandar­asi hiyo.

Mshambuliaji wa Simba, Haruna Niyonzima akiopambana na wachezaji wa Simba.

Hivyo, atakuwa na kibarua kigumu kuhakikisha anafanikiwa kushinda mchezo huo ambao utakuwa na upinzani mkubwa.

KILA TIMU ITAHITAJI KUKAA KILELENI

Simba na Yanga zimefungana katika msimamo wa ligi kuto­kana na zote kuwa na pointi 15, huku Simba ikiongoza kwa kuwa na idadi kubwa ya mabao ya kufunga. Simba ina mabao 19 na Yanga ina mabao 10.

 

Hivyo, kutokana na jinsi msi­mamo ulivyo, timu ambayo itashinda katika mchezo huo ndiyo itakayopata nafasi ya kuongoza msimamo wa ligi na iwapo itatokea wakatoa sare na Mtibwa Sugar yenye pointi 15 ikishinda mechi yao ya Ju­mapili dhidi ya Singida United basi itakaa kileleni.

KUONYESHANA UBORA WA VIKOSI

Kila timu inajinadi kuwa na kikosi bora ambacho imekisa­jili msimu huu, hivyo mashabiki wanasubiri kwa hamu kubwa kuona timu gani itaonyesha ufundi zaidi katika mchezo huo.

 

AJIBU, NIYONZIMA & OKWI VIVUTIO

Kwa sasa habari ya mjini ka­tika timu hizo ni kuhusiana na viwango vya wachezaji Ibrahim Ajibu wa Yanga na Haruna Niy­onzima na Emmanuel Okwi wa Simba, hivyo kila mmoja atahi­taji kuona wanafanya nini ka­tika mechi hiyo ya kesho.

Kwa upande wa Okwi, ndiye mchezaji kinara wa mabao kwenye ligi akiwa na mabao nane ambayo yameifanya kiko­si hicho kukaa kileleni kwa to­fauti ya mabao.

Aidha, wachezaji Ajibu na Niyonzima, kwa sasa ni gumzo kutokana na viwango wana­vyoonyesha. Mashabiki wa timu hizo wamekuwa waki­rushiana maneno huku wale wa Yanga wakidai Simba wamepoteza mchezaji (Ajibu) kwani amekuwa muhimu Jang­wani na Niyonzima akipondwa kwa kuonyesha uwezo wa ka­waida tofauti na ule aliokuwa akionyesha Yanga.

Mashabiki wa timu ya Yanga na Simba.

HOFU YA MASHABIKI

Hofu kubwa ya mashabiki kuelekea mchezo huo, itakuwa namna ya kuingia uwanjani kwani kwa muonekano wa haraka Uwanja wa Uhuru jinsi ulivyo hauwezi kukidhi mahitaji ya mashabiki kutokana na udo­go wa uwanja huo tofauti na ule wa Taifa ambao ni mkubwa.

Kuna uwezekano mkubwa kwa mashabiki wengi kuanga­lia mpira huo kupitia runinga kutokana na kushindwa ku­ingia uwanjani licha ya kuhitaji kuwaona wachezaji ‘live’ uwan­jani.

Makala – Bongo: Khadija Mngwai, Dar Es Salaam

 

Leave A Reply